Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rushine atuma salamu Yanga

RUSHINE Pict

Muktasari:

  • Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo wa dabi ya Kariakoo wa kwanza kwenye ligi msimu huu, utakaopigwa Oktoba 10, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mechi ambayo imeanza kupandisha joto kwa mashabiki wa timu zote.

SIMBA imerejea nchini ikitokea Afrika Kusini ilikoweka kambi yake ya siku 10 kujiandaa na mchezo wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, sasa beki na nahodha wa timu hiyo Rushine De Reuck amenyoosha maelezo juu ya mchezo huo.

Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo wa dabi ya Kariakoo wa kwanza kwenye ligi msimu huu, utakaopigwa Oktoba 10, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mechi ambayo imeanza kupandisha joto kwa mashabiki wa timu zote.

Wekundu hao waliweka kambi hiyo nchini Afrika Kusini kwenye jiji la Polokwane, ikijiandaa na mechi hiyo kisha ikapata mechi mbili za kirafiki za kujipima ikipoteza zote mbili.

RUSH 01

Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kuwasili nchini Rushine alisema kuwa kambi yao ya Afrika Kusini imekuwa na mafanikio ambapo wamepata muda wa kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Yanga kwa utulivu mkubwa.

Rushine ambaye ndiye atawaongoza wachezaji wenzake kwenye mechi hiyo, wakati huu nahodha mkuu Shomari Kapombe akiwa majeruhi alisema kikosi hicho kipo tayari na kwamba wana kiu ya matokeo ya aina moja tu kutafuta ushindi.

Beki huyo raia wa Afrika Kusini, alisema wanafahamu kwamba wanakwenda kukutana na Yanga yenye ubora lakini kuna hesabu wamezifanya wakiwa Afrika Kusini ndio ambazo zitakwenda kuwapa matokeo ambayo wanataka viongozi na mashabiki wao.

“Bila shaka tumepata muda mzuri wa kujiandaa, tupo tayari kwa mchezo huu, tumekuwa na wakati mzuri wa kujiandaa kama timu nadhani itatupa faida katika mechi zinazofuata hasa huu wa dabi ni mechi ngumu lakini tutafanya vizuri,” alisema Rushine.

RUSH 02

“Kuna mambo tumejiandaa nayo kwenye mechi hiyo, nadhani yatatupa matokeo mazuri ambayo viongozi na  mashabiki wetu wanayataka, tunahitaji ushindi tu ili kulinda heshima ya klabu yetu, tunaweza kufanya hivyo.

Naye kocha wa timu hiyo, Steve Barker ambaye alirejea nchini kitofauti na wachezaji wake alisema mashabiki wao wala hawana sababu ya kuingia ubaridi na matokeo ya kupoteza mechi walizocheza za kirafiki.

“Hakuna sababu ya mashabiki wetu kufikiria kuhusu matokeo ambayo tuliyapata kule Afrika Kusini, kuna mambo ya msingi zaidi tulikuwa tunazingatia katika mech hizo kuliko kuangalia matokeo ya mwisho, tuna hesabu zetu,” alisema Barker.

“Kitu kinachonifurahisha ni namna wachezaji walivyojituma katika mazoezi yale na kila mmoja anataka kufanya kitu tofauti, tumerudi mapema ili kuendelea na maandalizi yetu tukiwa hapa, kila mmoja yupo sawa, tunataka kuwa na kiwango tofauti.”