Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila amkubali Shalulile, akabidhiwa kadi ya uanachama Yanga

CHALAMILA Pict

Muktasari:

  • Jina hilo la Shalulile lilitokana na Yanga kumsajili mshambuliaji Peter Shalulie ambaye atawasili nchini kuanza maisha mapya na klabu hiyo bingwa Tanzania, akitokea kwa Mabingwa wa Afrika, Mamemodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameibua shangwe kwenye mkutano mkuu wa Yanga kwa kukubali jina lake kubadilishwa huku pia akiomba kupewa rasmi kadi ya uanchama wa klabu hiyo ambapo zoezi hilo lilifanyika kwa haraka.

Wakati Chalamila akikaribishwa tu na kutambulishwa na mshehereshaji wa mkutano huo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, akampa jina mkuu huyo wa Mkoa akimuita Albert Shalulile Chalamila, huku wanachama wakishangilia ukumbini. 

Chalamila ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa Yanga unaofanyika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, wakati akitoa salamu zake akaanza kwa kulikubali jina hilo alilopewa akiwapongeza viongozi wa Yanga kwa namna wanavyoendelea kujenga timu imara.

Jina hilo la Shalulile lilitokana na Yanga kumsajili mshambuliaji Peter Shalulie ambaye atawasili nchini kuanza maisha mapya na klabu hiyo bingwa Tanzania, akitokea kwa Mabingwa wa Afrika, Mamemodi Sundowns ya Afrika Kusini.

"Kwa kuwa mmenipa jina hili na wewe Rais (Hersi Said) umeridhia, nami nalikubali kwa kuwa naona namna mambo mazuri yanayoendelea kufanyika, wachezaji kama hawa wataendelea kuipa heshima nchi yetu," amesema Chalamila.

Aidha, wakati Chalamila akiendelea kuwahutubia wanachama wa Yanga, alisema anapata raha zaidi wakati Yanga ikifanya vizuri huku akiomba kadi ya uanachama wa klabu hiyo.

Chalamila amesema ameamua kufanya hivyo ikiwa ni kumuunga mkono marehemu William Lukuvi ambaye alisimamia mazishi yake alipofariki dunia  Machi 25, 2026.

"Nimemuona hapa marehemu Lukuvi alikuwa mwanachama wa klabu hii na mimi nilisimamia mazishi yake, nadhani ni wakati sasa kuwa mwanachama kamili.

"Nimeona hamnipi hii kadi sasa nadhani ni wakati wa mimi kuungana na kiongozi wetu kama kepteni Mkuchika ambaye atafurahi akiniona najiunga na klabu hii.

"Mimi ni mkuu wa Mkoa, zinapofanya vizuri klabu zingine huwa nafurahi sana lakini ukweli ni kwamba Yanga inaposhinda huwa nafurahi zaidi," amesema Chalamila.

Ndani ya dakika 20, Chalamila akakabidhiwa kadi yake ya uanachama na Rais wa Yanga, Hersi Said.

Aidha Chalamila amewataka wanachama wa Yanga kuendelea kuwa watulivu kwa kuimarisha amani akiwataka kuendelea kufanya vizuri kwenye soka nchini.