Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BTMZ, ZFF waungana kuinua vwango vya makocha Zanzibar

MAKOCHA Pict

Muktasari:

  • Hayo aliyasema wakati akizindua mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong. Amesema maendeleo ya soka yanategemea uwekezaji katika elimu kwani ndio msingi wa kuendeleza vipaji vya wachezaji.

NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, amesema mafunzo ya utimamu wa mwili kwa makocha ni hatua muhimu ya kuongeza ubora wa soka nchini.

Hayo aliyasema wakati akizindua mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong. Amesema maendeleo ya soka yanategemea uwekezaji katika elimu kwani ndio msingi wa kuendeleza vipaji vya wachezaji.

Hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuyatumia kikamilifu ili kuimarisha uwezo wao wa kitaaluma na kuinua kiwango cha mchezo.

Amesema, michezo ni chanzo kikubwa cha ajira, uchumi na maendeleo, hivyo ni muhimu kwa makocha kuendelea kujifunza mbinu mpya zitakazowajengea wachezaji uwezo wa kiufundi na utimamu wa mwili unaohitajika katika ushindani wa kisasa.

“Mafunzo haya sio ya kuhudhuria tu kwa ajili ya kupata cheti au kupiga picha, bali ni fursa ya kujifunza mambo mapya yatakayoimarisha utendaji wenu na kuongeza thamani yenu katika taaluma ya ukocha,” amesema.

Aidha aliipongeza Serikali kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya miundombinu ya michezo na kuweka mazingira bora ya kukuza vipaji vya vijana.

Awali, Katibu wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), Hussein Ahmada Vuai, amesema mafunzo ya utimamu wa mwili ni nguzo muhimu katika maandalizi ya timu na yatawasaidia makocha kuwajengea wachezaji uwezo wa kucheza kwa kiwango cha juu kwa dakika zote 90 za mchezo.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Said Kassim Marine, amesema mafunzo ni sehemu muhimu ya maendeleo ya michezo na kwamba bila kuwawezesha makocha kupitia mafunzo ya mara kwa mara, itakuwa vigumu kufikia viwango vya ushindani wa kimataifa.