Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ben anavyoitafuta nafasi Taifa Stars

BEN Pict

Muktasari:

  • Starkie ameonyesha dalili za kurejea kwenye ubora wake baada ya kufunga mabao manne katika michezo mitatu ya mwisho aliyoanza kikosi cha kwanza.

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Ben Starkie ameendelea kuonyesha kiwango bora kwenye kikosi cha Truro City ya England ambako yuko kwa mkopo akitokea Harborough Town FC ya nchi hiyo.

Starkie ameonyesha dalili za kurejea kwenye ubora wake baada ya kufunga mabao manne katika michezo mitatu ya mwisho aliyoanza kikosi cha kwanza.

Kiwango hicho kinaashiria kurejea kwenye ubora wake katika eneo la ushambuliaji na kumpa nafasi ya kuendelea kujenga ushindani ndani ya kikosi hicho ambako yupo kwa ajili ya kurejesha makali yake.

Mafanikio hayo yanakuja baada ya kiungo huyo kupitia kipindi kigumu msimu uliopita, alipokabiliwa na majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu. Hali hiyo ilimnyima nafasi ya kucheza mara kwa mara, lakini sasa anaonekana kurejea taratibu. 

BEN 01
BEN 01

Mabao hayo manne yanaweza kuwa hatua muhimu kwa Starkie katika safari ya kuimarisha nafasi yake Truro City na kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Mbali na klabu yake, pia kiwango hicho kinaweza kumuweka kwenye nafasi nzuri ya kurejeshwa tena Taifa Stars iliyo chini ya Kocha Miguel Gamondi ambaye amekuwa akiwaita nyota wanaokiwasha nje.

Starkie aliichezea Taifa Stars kwa mara ya kwanza Machi 24, 2022, katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo Tanzania ilishinda kwa mabao 3-1.

Pia aliwahi kuwa sehemu ya kikosi cha Tanzania cha vijana chini ya miaka 23 kilichoshiriki michezo ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini Septemba 2022.