Beki Yanga apewa madini

Muktasari:

BEKI wa Yanga, Dickson Job ni miongoni mwa nyota wanaokuja kwa kasi nchini kwa sasa katika beki ya kati, lakini kuna baadhi ya nyota wa zamani wamemuangalia na kuamini kuna madini anayohitaji kuwa nayo ili awe mtamu zaidi katika kukabiliana na washambuliaji sambamba na kulilinda lango lake.

BEKI wa Yanga, Dickson Job ni miongoni mwa nyota wanaokuja kwa kasi nchini kwa sasa katika beki ya kati, lakini kuna baadhi ya nyota wa zamani wamemuangalia na kuamini kuna madini anayohitaji kuwa nayo ili awe mtamu zaidi katika kukabiliana na washambuliaji sambamba na kulilinda lango lake.

Job aliyesajiliwa Yanga kwenye dirisha dogo la msimu uliopita amekuwa mmoja ya mabeki wa kati tegemeo, akitumikishwa pia timu ya taifa na kucheza kwa ufanisi, lakini amekuwa akifafanishwa na beki wa zamani wa kimataif aliyekipiga Pamba, Sinmba na Taifa Stars, George Masatu. Hata hivyo, Masatu amemchambua Job na kusema anafurahi kuona akifananishwa naye, japo alisema ana makosa mambo matatu ya kuwa imara zaidi kama ilivyokuwa enzi akicheza, akiwa mmoja ya mabeki waliokuwa wagumu kupitika licha ya kuwa na umbo dogo kama Job.,

Akizungumza na Mwanaspoti, Masatu alisema Job anatakiwa kufanya mambo matatu ili afuate nyayo zake kwa kukufuata nyayo zake.

Masatu aliyataja ni kupiga kelele na wachezaji wake, awe karibu kuwasiliana na kipa na kuipanga safu yake ya ulinzi ili kutotoa mwanya wa washambuliaji kuipita.

Alisema, akiyafanyia kazi mambo hayo kwenye eneo lake ni bonge la mchezaji na mwenye uwezo mkubwa.

“Nia ya kumtaka awasiliane mara kwa mara na kipa wake ni kutokana na kipa kuuona uwanja wote hivyo akiwasiliana nae muda mwingi itasaidia kuipanga timu yake,” alisema Masatu na kuongeza kuwa anatakiwa kutotakata tamaa kupambana.

Alisema mbali na kuisaidia Yanga anaamini hata timu ya Taifa ataisaidia. Job alikuwa mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa kikosi cha kwanza cha kocha Nasreddine Nabi katika michezo miwili dhidi ya Geita na Kagera Sugar.