Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Singida Black Stars achekelea ushindani

KAZI Pict

Muktasari:

  • Msimu uliopita wa 2025/26, alijiunga na Namungo FC akitokea Simba, alifanikiwa kuandika rekodi ya kuongoza kucheza dakika nyingi 2700, jambo analolichukulia kama chalenji katika ligi ya msimu wa 2026/27.

BEKI wa Singida Black Stars, Hussein Kazi amesema kutokana na ushindani wa namba uliopo katika timu hiyo, unampa chachu ya kujituma kwa bidii, kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza na kuendeleza alichokifanya msimu uliopita.

Msimu uliopita wa 2025/26, alijiunga na Namungo FC akitokea Simba, alifanikiwa kuandika rekodi ya kuongoza kucheza dakika nyingi 2700, jambo analolichukulia kama chalenji katika ligi ya msimu wa 2026/27.

Kazi baada ya kujiunga na SBS alifanikiwa kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) iliyopigwa Juni 9, 2026 dhidi ya Al Ghazala nchini Sudan Kusini, timu hiyo ikishinda kwa mabao 7-1, amesema bado hajapata nafasi ya kucheza mechi za ligi ya ndani.

“Ni timu mpya tayari kuna mabeki walioonyesha ushindani na kiwango cha juu, hiyo nachukua kama chalenji ya kupambana na kuhakikisha kiwango changu kinakuwa na muendelezo mzuri,” amesema Kazi na kuongeza;

“Katika nafasi ninayocheza kuna mabeki kama Abdulmalik Zakaria, Kennedy Juma na Benjamin Tanimu, hao ni chalenji nzuri sana kwangu, kujituma na kutobweteka.”

Kazi amesema siyo jambo geni kukutana na ushindani akitolea mfano wa Simba kipindi ambacho hajaumia Abdulrazack Hamza alikuwa ni kati ya mabeki ambao alikuwa anampa nguvu ya kujituma:”

Mchezaji anayependa kufika mbali, hawezi kuogopa ushindani ambao utamjenga kuwa bora, ndiyo maana nafurahia chalenji nzuri niliyokutana nayo Singida.”