Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki mpya Azam FC afichua jambo

BEKI Pict

Muktasari:

  • Beki huyo anayefahamika kwa jina la utani la The Destroyer, amewasili Chamazi akiwa na matumaini makubwa ya kuisaidia Azam kutimiza malengo yake ya kupigania mataji ya ndani na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

AZAM FC imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2026-2027 baada ya kumtangaza rasmi beki wa kati raia wa Ubelgiji, Henri Stanic, aliyesajiliwa kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.

Beki huyo anayefahamika kwa jina la utani la The Destroyer, amewasili Chamazi akiwa na matumaini makubwa ya kuisaidia Azam kutimiza malengo yake ya kupigania mataji ya ndani na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Mara baada ya kutambulishwa, Stanic amesema hakuhitaji muda mrefu kufikiria ofa ya Azam kwa sababu tayari alikuwa akifuatilia maendeleo ya soka la Tanzania na aliamini ulikuwa wakati sahihi kwake kuanza changamoto mpya katika maisha yake ya soka.

“Nadhani haikuchukua muda mrefu kufanya uamuzi. Nilijua kuhusu Ligi Kuu Tanzania na ushindani wake. Ni moja ya ligi zinazokuwa kwa kasi na niliona huu ndiyo wakati sahihi kwangu kujaribu changamoto mpya,” amesema Stanic.

Beki huyo amesema amevutiwa na kiwango cha ushindani kilichopo kati ya klabu kubwa nchini, jambo ambalo linaifanya ligi kuwa na mvuto kwa wachezaji kutoka mataifa mbalimbali.

“Ninapenda kushindana katika mazingira yenye ushindani mkubwa. Hilo ndilo lililonivutia zaidi. Ninaamini kujiunga na Azam kutanifanya niendelee kukua kama mchezaji na wakati huohuo kuisaidia timu kufikia malengo yake.”

Stanic anaingia Azam akitokea Stellenbosch FC, klabu ambayo imeendelea kujijengea heshima katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa kupambana na vigogo kama Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates na Kaizer Chiefs.

Akiwa Afrika Kusini, beki huyo alijulikana kwa uimara wake wa kuzuia mashambulizi, uwezo mzuri wa kucheza mipira ya juu pamoja na utulivu wa kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma, sifa zilizompatia jina la The Destroyer.

Azam imekuwa ikifanya maboresho makubwa ya kikosi chake baada ya msimu uliopita kumaliza katika nafasi za tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, hivyo kushindwa kufikia malengo yake ya kutwaa ubingwa, huku kwa upande wa Kombe la CRDB ikipoteza fainali dhidi ya Simba.

Uongozi wa klabu hiyo unaamini ujio wa Stanic utaongeza ushindani katika safu ya ulinzi ambayo imekuwa moja ya maeneo yaliyolengwa kuimarishwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Mbali na uwezo wake wa kukaba, Stanic pia anatajwa kuwa beki mwenye uongozi mkubwa uwanjani kutokana na uzoefu alioupata katika ligi mbalimbali za Ulaya na Afrika Kusini.