Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipre Junior namuwekea dhamana Azam

KIPRE Pict

Muktasari:

  • Baada ya kucheza katika Ligi Kuu ya Algeria kwa misimu miwili mfululizo akiitumikia MC Alger, Kipre Junior amerudi katika timu yake ya zamani ya Azam FC aliyoachana nayo mwaka 2024.

HATIMAYE mtoto amerejea nyumbani. Ni Kipre Zunon ambaye kwa hapa nchini amezoeleka kwa jina la Kipre Junior.

Baada ya kucheza katika Ligi Kuu ya Algeria kwa misimu miwili mfululizo akiitumikia MC Alger, Kipre Junior amerudi katika timu yake ya zamani ya Azam FC aliyoachana nayo mwaka 2024.

Kwa hapa kijiweni, usajili wa mchezaji kama Kipre Junior hauwezi kutupa wasiwasi na wengi sana tumeiunga mkono Azam FC kumrudisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Kwanza anarudi nchini akiwa sio mchezaji aliyefeli ndani ya uwanja kule Algeria kwani amecheza idadi kubwa ya mechi za mashindano tofauti ambazo ameitumikia MC Algeria.

Takwimu zinaonyesha katika misimu miwili aliyoichezea timu hiyo ya Algeria, winga huyo amecheza idadi ya mechi 76 za mashindano tofauti na kati ya hizo, 48 alianza kikosini na 28 alitokea benchi.

Kwa nchi kama Algeria, mchezaji akiweza kupata nafasi ya kucheza wastani wa mechi 38 kwa msimu, huyo maana yake hakuwa msindikizaji kikosini na badala yake alikuwa muhimu.

Kingine ni kwamba Kipre Junior anarudi katika nchi na klabu ambayo anaifahamu vyema na mazingira pamoja na utamaduni wake, hivyo hatokuwa na utetezi au kusema hajazoea soka la hapa.

Na pia anarudi katika umri ambao bado unamruhusu kucheza kwa ushindani wa hali ya juu kwani mwili wake bado haujachoka na anaweza kuendana na kasi ya mechi.

Usajili wa Kipre Junior ni jambo ambalo huwezi kuibeza Azam FC kwa kulifanya kwani wote tunaujua uwezo wa mchezaji huyo labda mambo yakatae tu.