Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker afunga njia Simba

BARKER Pict


UKIWASIKILIZA mashabiki wa Simba, ni kama wanaona timu yao inashinda kwa shida. Lakini ukifika uwanjani, unakutana na timu tofauti ambayo imeshinda kibabe.


Kuna baadhi ya mabao ya ufundi sana ambayo yanatokana na kazi inayofanyika mazoezini. Hapa ndipo sehemu inayoonyesha Kocha Steve Barker na wenzake wanaibua tishio jipya.


Simba imecheza mechi tano kwenye ligi hadi sasa na kushinda zote, ikiwa katika nafasi ya pili na pointi 15, sawa na vinara Yanga, lakini ikiwa nyuma kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika mechi dhidi ya Pamba Jiji, Simba ilishinda mabao 2-1. Ukiitazama kwa umakini bao la kwanza, utaona ufundi mkubwa uliofanyika. Shambulizi hilo lilianza kutoka eneo la ulinzi na kuonyesha wazi kazi inayofanyika katika kutengeneza mashambulizi mazoezini.

Pasi zilipigwa kuanzia nyuma, kutoka kwa walinzi kwenda eneo la kiungo, kisha mpira ukapelekwa eneo la mwisho huku ukipita kwenye pande zote za uwanja. Hatimaye, Libasse Gueye alipiga krosi iliyomkuta Anicet Oura, aliyeuweka mpira wavuni kwa kichwa.

BAK 03

Wekundu hao walitengeneza bao hilo kwa kupiga pasi 16, kiwango cha ubunifu ambacho si rahisi kukiona kwenye ligi.

Kama haitoshi, juzi dhidi ya Geita Gold, Simba ilirudia jambo hilo ilipofunga bao la kwanza katika ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0. Bao hilo pia lilitengenezwa kwa ubora mkubwa, likianzia eneo la ulinzi.

BAK 02

Wachezaji wa timu hiyo walipiga pasi 10 kuanzia nyuma, zikafika eneo la kiungo na hatimaye katika robo ya mwisho ya uwanja. Gueye alipiga tena krosi iliyomkuta kiungo Clatous Chama, ambaye alifunga kwa ufundi wa hali ya juu.

Mabao haya mawili yanatoa picha kwamba kuna kazi kubwa ya kiufundi inayofanyika kwenye uwanja wa mazoezi, na wachezaji wa timu hiyo wanaelewa kile wanachofundishwa na kwenda kukifanyia kazi uwanjani wakati wa mechi.

Simba katika mechi za msimu huu imekuwa ikitumia viungo wengi wenye uwezo wa kuchezesha zaidi badala ya wale wakabaji, ambao wamekuwa wakiingia kipindi cha pili ili kuimarisha ulinzi na kuulinda ushindi.

BAK 01

Katika mchezo wa juzi dhidi ya Geita Gold, Simba ilianza na viungo watano ambao ni Neo Maema, Libasse Gueye, Morrice Abraham, Clatous Chama na Anicet Oura. Wote wana uwezo mkubwa wa kushambulia kuliko kulinda, huku Yusuf Kagoma, ambaye asili yake ni kiungo mkabaji, akiingia kipindi cha pili.

Akizungumzia hilo, kocha wa Simba, Steve Barker, aligoma kuweka wazi mbinu zake, akisema anafurahishwa na namna wachezaji wake wanavyozidi kuimarika katika kutengeneza ushindi kwenye mechi za timu hiyo.

“Siwezi kuweka wazi sana mikakati yetu ya kutengeneza ushindi, hiyo ni siri yetu. Lakini pongezi zangu ni kwa wachezaji wanavyozidi kuimarika katika kutengeneza ushindi kwenye mechi zetu. Kuna ukomavu mzuri unaoonyeshwa.”