Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca, Destiny wanavyotengeneza balaa La Masia

BARCA Pict

Muktasari:

  • Vijana hao, Destiny Kosiso kutoka Nigeria na Barka Seif, raia wa Tanzania, wamekuwa kivutio kikubwa kutokana na kiwango bora wanachokionyesha kwenye akademi hiyo.
  • Kinda wa Tanzania, Seif ambaye alijiunga na akademi hiyo msimu huu akitokea CF Damm, kwenye mechi mbili za ligi ya vijana U-12 alifunga mabao manne.

WAKATI nyota mwenye asili ya Afrika, Lamine Yamal akiendelea kuwaka kwenye kikosi cha Barcelona, kuna balaa lingine la makinda wa Afrika linatengenezwa kwenye kikosi cha La Masia.

Vijana hao, Destiny Kosiso kutoka Nigeria na Barka Seif, raia wa Tanzania, wamekuwa kivutio kikubwa kutokana na kiwango bora wanachokionyesha kwenye akademi hiyo.

Kinda wa Tanzania, Seif ambaye alijiunga na akademi hiyo msimu huu akitokea CF Damm, kwenye mechi mbili za ligi ya vijana U-12 alifunga mabao manne.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kijana huyo wa Kitanzania ana wastani wa kufunga mabao mawili kila mechi, jambo linalothibitisha ubora wake anapokuwa eneo la hatari la mpinzani.

Lakini huo ni muendelezo tu kwani akiwa CF Damm, Barka alionyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao, akimaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji baada ya kutikisa nyavu mara 41 katika mechi 28 za ligi ya vijana.

Destiny Kosiso naye  amekuwa gumzo kubwa baada ya kupachika mabao nane katika mechi nne pekee za ligi alizocheza hadi sasa. Kasi yake ya kufumania nyavu, nguvu na uwezo wa kukaa kwenye nafasi sahihi umewafanya mabeki wa timu pinzani kupata tabu kubwa.

Wawili hawa wanaocheza kama washambuliaji wa kati wameonyesha uelewano wa hali ya juu na kuifanya safu ya ushambuliaji ya La Masia kuwa moja ya safu hatari zaidi katika ligi hiyo ya vijana.

Ni wazi kuwa uwepo wao kikosini unatoa taswira nzuri ya vipaji vinavyotoka barani Afrika na kupikwa vyema kwenye vyuo vya soka barani Ulaya.