Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yamal, Messi mechi tisa zinazokaribiana

MESSI Pict

Muktasari:

  • Tangu Yamal alipoanza kukipiga katika kikosi hicho akiwa na umri wa miaka 15 amekuwa akilinganishwa na Messi. Hata hivyo, mara nyingi ulinganisho huo umeonekana kuwa usio wa haki kutokana na ukubwa wa mafanikio ya nyota wa kimataifa wa Argentina ambayo ni vigumu kwa mchezaji mwingine kuyafikia.

BARCELONA, HISPANIA: KUNA jambo la kipekee linaloendelea kwa winga wa Barcelona, Lamine Yamal kadiri mwanzo wake wa msimu wa 2026/27 unavyozidi kuwa wa kuvutia, kwani ndivyo inavyokuwa vigumu kuepuka ulinganisho wake na supastaa wa zamani wa timu hiyo, Lionel Messi.

Tangu Yamal alipoanza kukipiga katika kikosi hicho akiwa na umri wa miaka 15 amekuwa akilinganishwa na Messi. Hata hivyo, mara nyingi ulinganisho huo umeonekana kuwa usio wa haki kutokana na ukubwa wa mafanikio ya nyota wa kimataifa wa Argentina ambayo ni vigumu kwa mchezaji mwingine kuyafikia.

“Mimi sijilinganishi naye (Messi), kwa sababu sijilinganishi na mtu yeyote, sembuse Messi,” kinda huyo wa Barcelona aliwaambia waandishi wa habari mwaka 2025. “Sidhani kama ulinganisho huo una maana, hasa inapohusu Messi. Mimi nitafurahia kucheza na kuwa mwenyewe.”

Hata hivyo, kufanana kwa safari zao za soka kunazidi kuonekana. Yamal, tayari ameshinda ubingwa wa Ulaya na Kombe la Dunia 2026 akiwa na Hispania, mataji mawili mfululizo ya La Liga akiwa na Barcelona na pia amewahi kumaliza nafasi ya pili katika tuzo za Ballon d’Or. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba bado ana umri wa miaka 19. Ukiangalia kwa jicho la takwimu, Yamal amefika hatua kubwa zaidi katika umri huo kuliko Messi alivyokuwa amefikia akiwa katika umri na hatua hiyo hiyo ya maisha yake ya soka Barcelona.


MESS 03

Msimu wa 2008/09 mwanzo enzi za Messi

Kuna mfanano wa kuvutia kati ya mahali Yamal alipo sasa na hali aliyokuwa nayo Messi katika majira ya kiangazi 2008. Wote walikuwa tayari wamejijengea nafasi miongoni mwa wachezaji bora duniani na walikuwa wamemaliza nafasi ya pili katika tuzo za Ballon d’Or.

Messi alimaliza nyuma ya Cristiano Ronaldo, jambo lililoashiria mwanzo wa ushindani mkubwa kati ya nyota hao wawili ambao ulitawala soka la dunia kwa zaidi ya muongo mmoja. Kwa upande wake, Yamal alimaliza nyuma ya Ousmane Dembele katika tuzo za mwaka uliopita. Kwa sasa, kampuni za ubashiri zinamtabiria kumaliza tena nafasi ya pili, safari hii nyuma ya Harry Kane.

Mchezaji huyo aliyelelewa katika akademi ya La Masia alikuwa tayari anang’ara kabla Pep Guardiola hajawa kocha wa Barcelona. Katika msimu wa 2007/08, Messi alifunga mabao 13 na kutoa asisti 16. Hizo zilikuwa takwimu nzuri, ingawa hazikuonyesha kikamilifu uwezo wake mkubwa.

Kisha ukafika msimu wa 2008/09, ambao Barcelona ilitwaa mataji matatu makubwa. Guardiola alijenga kikosi kilichomwezesha Messi kuonyesha uwezo wake wote, na Muargentina huyo akajibu kwa kufunga mabao 38 katika msimu huo.

MESS 01

Huo ndio uliokuwa msimu ambao Messi alianza kuonekana kuwa mchezaji asiyezuilika. Baadaye alishinda tuzo nane za Ballon d’Or na kuanza kutajwa pamoja na Pele na Diego Maradona katika mijadala ya wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka.

Yamal naye amekuwa akionyesha kiwango cha juu, ingawa bado hajazalisha mara kwa mara takwimu za kuvutia kama zile ambazo Messi alizifikia katika kilele cha uwezo wake. Hata hivyo, mabao nane na asisti saba katika mechi zake tisa za kwanza za msimu wa 2026/27 vinaashiria huenda jambo kubwa linaanza kubadilika. Huo ni mwendelezo wa hatua muhimu ikilinganishwa na mchango wake katika misimu iliyopita.

Jambo linalovutia zaidi ni kwamba Yamal kwa sasa ana mchango mkubwa zaidi wa mabao kuliko Messi aliokuwa nao katika mechi zake tisa za mwanzo za msimu wa 2008/09 chini ya Guardiola. Katika mechi hizo, Messi alifunga mabao manane na kutoa asisti tano.

Bila shaka, msimu bado ni mchanga. Lakini ikiwa Yamal ataendelea kucheza kwa kiwango kinachokaribia hiki, huenda kumaliza nafasi ya pili katika Ballon d’Or tena kukawa hatua ya mwisho kabla ya kuanza enzi yake ya kutawala soka la dunia.

Hizi hapa takwimu za Yamal na Messi baada ya kila mmoja kucheza mechi tisa za mwanzo za msimu husika.


MESS 04

NAMBA ZAO

Yamal katika mechi tisa za mwanzo msimu wa 2026/27 amefunga mabao manane, asisti saba akiwa na mchango wa mabao 15 hadi sasa, huku akifunga bao moja la penalti akiwa na uwiano wa kufunga bao kila baada ya dakika 96, ilhali dakika zake kwa bao lisilotokana na penalti ni 95 na kwa maana nyingi dakika kwa kila bao au asisti ikiwa ni 50

Kwa upande wa Messi katika mechi tisa za mwanzo 2008/09 alifunga mabao manane, asisti tano akichangia mabao 13 ya Barcelona, huku akitupia mawili kwa penalti na uwiano wa dakila kwa kila bao ukiwa 83. Hata hivyo kwa alikuwa na dakika kwa kila bao lisilotokana na penalti  111, ilhali dakika kwa kila bao au asisti ikiwa ni 51.


MESS 02

ULINGANGANISHO UNAONYESHA NINI?

Yamal na Messi wamefunga mabao manane kila mmoja baada ya mechi tisa. Hata hivyo, Yamal ametoa asisti saba dhidi ya tano za Messi, hivyo kufikisha jumla ya michango 15 ya mabao, huku Messi akiwa na 13.

Pia, Yamal ana wastani wa dakika 50 kwa kila bao au asisti, ikilinganishwa na dakika 51 za Messi. Kwa upande mwingine, Messi alifunga kwa kasi zaidi akitumia wastani wa dakika 83 kwa kila bao dhidi ya 96 za Yamal. Takwimu hizi zinaonyesha mwanzo mzuri wa Yamal, lakini bado ni mapema mno kutabiri kama ataweza kufikia mafanikio ya Messi. Kinachovutia ni kwamba, akiwa na umri wa miaka 19, tayari anaweka takwimu zinazochochea ulinganisho na mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi katika historia ya soka.