Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda mtanzania ang'ara Barca

BARKA Pict

Muktasari:

  • Barka alivutia katika mashindano hayo yanayokutanisha vijana kutoka akademi mbalimbali za soka barani Ulaya, akifunga mabao matatu na kutoa asisti moja katika michezo miwili aliyocheza.

KINDA wa Kitanzania, Barka Seif, anayecheza katika akademi ya FC Barcelona, La Masia, Hispania, ameendelea kung’ara baada ya kuchaguliwa katika kikosi bora cha wiki cha mashindano ya vijana ya Virgil Legacy Trophy.

Barka alivutia katika mashindano hayo yanayokutanisha vijana kutoka akademi mbalimbali za soka barani Ulaya, akifunga mabao matatu na kutoa asisti moja katika michezo miwili aliyocheza.

Katika michezo hiyo, Barka alifunga bao moja dhidi ya Chelsea, kabla ya kuongeza mabao mawili na kutoa asisti moja Barcelona ilipokutana na Willem II ya Uholanzi.

Mchango wake uliisaidia Barcelona kumaliza hatua ya makundi ikiwa kinara wa Kundi A, lililokuwa pia na Chelsea na Galatasaray.

BARK 01

Kiwango hicho ni mwendelezo wa safari ya kinda huyo, ambaye kipaji chake kilianza kuonekana akiwa na umri mdogo.

Mwaka 2021, akiwa na miaka saba, Barka alishiriki kliniki za soka za vijana zilizoandaliwa na akademi ya Ajax Amsterdam nchini Uholanzi, kabla ya kujiunga na CF Damm, akademi iliyopo Catalonia, Hispania.

Akiwa CF Damm, Barka alionyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao, akimaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji baada ya kutikisa nyavu mara 41 katika mechi 28 za ligi ya vijana.

BARK 02

Machi 2026, alichaguliwa pia katika kikosi bora cha vijana chini ya miaka 12 cha Shirikisho la Soka la Catalonia, baada ya kufunga mabao 18 katika mechi 20 za ligi.

Juni mwaka huu, Barka alijiunga na La Masia, akademi inayojulikana kwa kukuza vipaji vya soka duniani, wakiwamo Lionel Messi na Lamine Yamal.

Hatua hiyo imeongeza matumaini ya kuona kinda huyo akiendelea kupiga hatua katika soka la vijana, huku akiwakilisha Tanzania katika mazingira yenye ushindani mkubwa wa soka la Ulaya.