Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI apewa Uzi wa Pacome, atangaza vita CAF

Muktasari:

  • Yanga iliandaa hafla maalumu ya mashabiki na viongozi wa klabu hiyo ikifanyika kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam ambapo licha ya kiingilio kuwa sh 2000 tu lakini mashabiki wakaujaza uwanja huo.

Yanga imemtambulisha rasmi kiungo Stephanie Aziz KI akirejea klabuni hapo baada ya kutambulishwa rasmi muda mfupi uliopita.

Yanga iliandaa hafla maalumu ya mashabiki na viongozi wa klabu hiyo ikifanyika kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam ambapo licha ya kiingilio kuwa sh 2000 tu lakini mashabiki wakaujaza uwanja huo.

Katika utambulisho huo Yanga ulisema itamtambulisha mchezaji X factor ambapo kama ambavyo Mwanaspoti lilikupa kila hatua ya usajili wake, staa huyo raia wa Burkina Faso akatambulishwa rasmi.

Wakati wa utambulisho huo Azizi KI ambayw ni mume wa mwanamitindo Hamisa Mobetto aliibuka wakati uwanja ukiwa umezimwa taa ambapo wakati zilipowashwa akaonekana akiwa jukwaa maalum akiwa na Rais wa Yanga injinia Hersi Said.

Aziz KI amesaini mkataba wa miaka miwili akirejea klabuni hapo baada ya kuuzwa Wydad Athletic ya Morocco, Kisha baadaye Waarabu hao kumuuza Al Ittihad ya Libya Kisha Yanga kumnunua tena kwa Dola 450,000.

Mara baada ya utambulisho huo Azizi KI akiwa amevalia jezi ya kijani ya msimu huu, zikapigwa fataki maalum kuonyesha ukaribisho huo.


KI APEWA UZI WA PACOME, ATANGAZA VITA CAF

Wakati Yanga ikimtambulisha kiungo Stephanie Aziz KI, uongozi wa klabu hiyo umemrudishia jezi namba 10 ambayo alikuwa akiitumia kabla ya kuachana na klabu hiyo.

Kwenye utambulisho huo ambao umefanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex, Aziz KI amekabidhiwa jezi hiyo na Rais wa Yanga injinia Hersi Said yenye namba 10 mgongoni.

Wakati Aziz KI akikabidhiwa jezi hiyo, nyeusi ya msimu huu, Meneja wa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema uamuzi huo umetokana na baraka za kiungo wao Pacome Zouzoua ambaye ameridhia jezi hiyo kutumiwa na staa huyo.

"Wakati taarifa hizi zilipomfikia kiungo wetu Profesa wa mpira Pacome Zouzoua, akamwambia Aziz KI we chukua hiyo jezi nenda kafanye balaa mi nikirudi nitatumia jezi ya namba 26, "amesema Kamwe huku akishangiliwa na mashabiki walijaa Uwanja mzima.

Pacome aliumia kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, ambapo Yanga imelazimika kumuondoa kwenye usajili wa msimu huu kutokana na hataweza kupona ndani ya msimu huu.

Mara baada ya utambulisho huo Aziz KI amesema amerejea nyumbani na kwamba anataka kuona Yanga inafanya vizuri mashindano ya Afrika msimu ujao.

"Ahsanteni sana Wananchi, Nina furaha sana kuwaona tena na kurudi hapa, Yanga Bingwa, nimeona tumeendelea kuwa Mabingwa kwa misimu mitano hapa nchini lakini sasa tunatakiwa kuchukua ubingwa wa Afrika,"amesema Aziz KI