Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yavunja rekodi ya Simba Afrika

Kocha wa Azam FC Stewart Hall akiendeleza kazi yake kwenye mazoezi ya viungo na stamina

MWANDISHI WETU SAHAU kuhusu uwanja wa kisasa wa Chamanzi unaomilikiwa na Azam au straika wake Muivory Coast Kipre Tchetche anayeongoza msimamo wa wafungaji Bara kwa mabao 16. Hapa inazungumziwa rekodi ya Afrika kwenye Kombe la Shirikisho na Mabingwa Afrika kuanzia miaka ya 2000. Azam imeifikia rekodi ya Simba kwa kucheza mechi tano za Kombe la Shirikisho bila kupoteza hata moja mpaka kufikia wikiendi iliyopita. Simba ilifanya hivyo mara ya mwisho kwenye Ligi ya Mabingwa mwaka 2003 ilipotinga hatua ya makundi. Simba ilicheza mechi tano bila kupoteza, mechi yake ya sita ilifungwa bao 1-0 na Zamalek ugenini zikaenda kwenye penalti Mnyama akashinda kwa penalti na kufuzu hatua ya makundi. Azam ambayo ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya kimataifa msimu huu, imecheza mechi tano ikashinda tatu na sare mbili. Azam inasubiri mechi ya marudiano dhidi ya FAR Rabat ya Morocco ugenini Mei 4 kuwania kufuzu hatua nyingine ya mtoano tayari kwa kuingia kwenye makundi. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Recreativo Libolo ya Angola imetoka suluhu na Enugu Rangers nchini Nigeria wikiendi iliyopita huku TP Mazembe ikifungwa mabao 3-1 na Orlando Pirates nchini Afrika Kusini bao la Mazembe likipigwa na Mulota Kabangu.