Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yaifuata Zed FC Misri

Muktasari:

  • Jumla ya nyota 24 wa kikosi cha Azam FC, wamesafiri kuelekea nchini Misri kuifuata timu ya Zed katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi cha timu ya Azam, kimeondoka leo Jumatatu asubuhi kuelekea jijini Cairo, Misri kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Zed.

Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Ijumaa, Oktoba 16, 2026, saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Azam FC itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kufika hatua ya makundi msimu uliopita wa 2025/2026 ambapo ilimaliza nafasi ya tatu katika kundi B ikiwa na pointi tisa nyuma ya Maniema iliyomaliza kwa pointi 12 wakati Wydad Athletic ikimaliza vinara kwa pointi 15.

AZA 01

Timu ya Zed ilifanikiwa kuvuka katika mchezo wa raundi ya kwanza baada ya kuitupa nje ASAS ya Djibouti kwa jumla ya mabao 5-1.

Zed ilipata ushindi wa mabao 4-0 ilipokuwa nyumbani kisha ikalazimishwa sare ya 1-1 katika mechi ya ugenini.

AZA 02

Hata hivyo, Azam FC nayo imekuwa na mwendelezo bora katika Ligi Kuu ambapo hadi sasa imecheza michezo nane ikiwa imeshinda mara tano, imetoka sare mechi mbili na kuruhusu kipigo kimoja ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 17.

Katika Ligi Kuu nchini Misri, Zed imecheza mechi tano hadi sasa ambapo imepata ushindi mara mbili, imetoka sare mara moja na kuruhusu vipigo viwili ikishika nafasi ya 11 kwa pointi saba.