Azam FC yabanwa mbavu Mapinduzi Cup
Azam FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Mlandege FC ambayo imetoka kucheza mechi ya kwanza ya mashindano hayo jana Julai 6.
Azam ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wao mpya Mpiana Mozizi akimalizia mpira wa kona uliomshinda beki wa Mlandege kuuondoa langoni.
Mozizi linakuwa bao lake kwa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili.
Mlandege ambao jana walitoka suluhu dhidi ya Malindi FC wamemaliza mechi zao za kundi C na kuvuna alama mbili sasa mechi iliyobaki na kati ya Azam dhidi ya Malindi.
Azam walianza mashabulizi mapema na dakika ya tatu walilisakama lango la Mlandege ila halikuza bao na Mpiana aliendelea kuwa mwiba kwa mabeki ila mashuti yake hayakuweza kuzaa lango.
Kwa upande wa Mlandege safu ya ushambiliaji ikiongozwa na nyota wao Rashid Mandawa ilitengeneza nafasi nyingi ambapo ukiachana na bao la kusawazisha alilofunga dakika 88 kwa kichwa walipata bao lingine ila mfungaji alikuwa ameotea.
Baada ya mechi hiyo nahodha msaidizi wa Azam, Frank Domayo alisema mipango yao ilikuw akupata alama tatu ila wapinzani wao walikamia mechi.
Upande wa Mlandege wamedai kucheza mechi mbili ndani ya siku mbili ni sababu ambayo imewafanya kuwa chini ya kiwango na kuvuna alama moja leo.
Simba itashuka dimbani kesho kuanza mechi ya kwanza dhidi ya Chipukizi kwenye kundi B na Yanga itatupa karata ya mwisho dhidi ya Namungo baada ya mechi ya kwanza kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Jamhuri.