Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asante Kotoko yaitibulia Yanga Afrika Kusini

YANGA Pict

Kama Yanga ilikuwa na mpango wa kutetea ubingwa wa Kombe la Toyota mwaka huu huko Afrika Kusini, umekufa rasmi baada ya waandaaji wa mashindano hayo kuialika timu ya Asante Kotoko ya Ghana.

Timu hiyo ya Ghana ndio itacheza kama mwalikwa katika mechi hiyo ambayo huwa dhidi ya wenyeji Kaizer Chiefs na sio Yanga ambayo ndio bingwa mtetezi wa kombe hilo.

Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Kaizer Chiefs, Jessica Motaung amefafanua kuwa mwaka huu, mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Moses Mabhida uliopo jiji Durban, Julai 26, 2025.

"Tunayo heshima kuwakaribisha marafiki zetu kutoka Ghana katika ardhi ya Afrika Kusini. Asante Kotoko ni sehemu ya historia yetu. Kombe la Toyota linaruhusu Waafrika kuungana na kusherehekea kumbukumbu zetu.

"Durban sio tu ni kitovu cha utengenezaji wa Toyota, Afrika Kusini, lakini ni mahali pazuri pa kuandika sura mpya ya historia yetu. Baada ya kushinda Kombe la Nedbank mwezi Mei katika Uwanja wa Moses Mabhida,” amesema Motaung.

Mwenyekiti wa Asante Kotoko, Apinkra Akwasi Awuah amesema wamefurahishwa na mualiko huo.

"Ni kwa furaha na matarajio makubwa kwamba tunakuja Afrika Kusini kwa toleo la 2025 la Kombe la Toyota. Kandanda daima imekuwa daraja la nguvu kati ya watu na mataifa, na tukio hili linaonyesha kile kinachowezekana wakati michezo inaungwa mkono na maono na madhumuni.

"Tunajivunia kuwa sehemu ya sherehe hii ya umoja wa Afrika na kupongeza Toyota na Kaizer Chiefs kwa kuweka kiwango cha soka cha Afrika," anasema Awuah.

Mwaka jana, Yanga ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo yalipofanyika kwa mara ya kwanza ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs.