Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaitekenya Cardiff mabao 3-2

England. Timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye uwanja wa ugenini na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuondoka na tabasamu zito uwanjani hapo.

Uamuzi wa Kocha wa Arsenal, Unai Emery kuwachezesha Pierre Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette tangu mwanzo wa mchezo imekuwa msaada wa timu hiyo na kuwafanya kuibuka na ushindi huo mnono.

Hadi timu hizo zinakenda mapumziko mabao yalikuwa 1-1 ambapo bao la Arsenal lilifungwa na Shkoran Mustafi dakika ya 11' huku bao la kusawazisha la Cardiff likiwekwa wavuni na Victor Camarasa dakika ya 45'.

Aubemameyang aliweka wavuni bao la pili dakika ya 62' huku Danny Ward akiisawazishia timu yake bao dakikaya 70'.

Msumari wa mwisho na bao la ushindi liliwekwa wavuni na Lacazette dakika ya 81' huku Harry Arter  wa Cardiff akiambulia kadi ya njano dakika ya 90'.