Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

19 zatinga hatua ya pili ZFF Cup Unguja

ZFF Pict

Muktasari:

  • Michezo hiyo ilianza Oktoba 22, 2026 na kuhitimishwa Oktoba 27, 2026, katika viwanja mbalimbali vya Unguja.

TIMU 19 zimefanikiwa kufuzu hatua ya pili ya michuano ya ZFF Cup, huku nyingine 19 zikiondolewa baada ya kukamilika kwa michezo ya hatua ya awali iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Michezo hiyo ilianza Oktoba 22, 2026 na kuhitimishwa Oktoba 27, 2026, katika viwanja mbalimbali vya Unguja.

Timu zilizofanikiwa kusonga mbele ni Urafiki, Negro United, Muembe Makumbi City, New Power, Mbuyuni, Flamingo, Ranger Bulls, Villa FC, Sebleni, Muungano Rangers, Nungwi City, Cairo United, Malindi, Kikungwi Star, Mbiji, Bridge Star, Mundu, Kitope na Scud SC.

Kwa upande mwingine, timu zilizoaga michuano hiyo ni Bweleo, Kundemba, New King, Ujamaa, Paje Star, Sungusungu, Pitanazako, Mwera, Sharp Boys, ZMCL, Black Lion, Maungani United, ZAFS Academy, Bububu, Nyangoro, New City, Zantex, New Academy na Ngome.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Khamis Ali Rashid, amesema michezo yote imekamilika vizuri bila changamoto kubwa kujitokeza.

Hata hivyo, Khamis amesema shirikisho hilo litaendelea kuwa makini katika kusimamia michuano hiyo ili kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki na kuzuia vitendo vya upangaji wa matokeo.

Amesisitiza kuwa usimamizi makini ni muhimu katika kulinda uadilifu wa mashindano na kuhakikisha timu zote zinapata nafasi ya kushindana kwa haki.

KMKM ndiyo bingwa mtetezi wa michuano hiyo, huku timu zinazofuzu hatua inayofuata zikijiandaa kuendeleza vita ya kuwania taji hilo.