Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anuary Jabir aweka lengo la kuvunja rekodi, kutwaa kiatu cha ufungaji

Muktasari:

  • Straika huyo anayekipiga Polisi Tanzania, ameonekana kuwa mwiba mkali akiwafunika mastaa wote Ligi Kuu kufuatia utupiaji mabao akifikisha matano na kukaa juu ya orodha ya wanaoongoza kutikisa nyavu.

ANUARY Jabir ambaye ana mabao matano katika Ligi Kuu Bara msimu huu, amesema anahitaji kuandika historia mpya na kuvunja rekodi za nyuma baada ya hapo awali kutokuwa na mwenendo mzuri.

Straika huyo anayekipiga Polisi Tanzania, ameonekana kuwa mwiba mkali akiwafunika mastaa wote Ligi Kuu kufuatia utupiaji mabao akifikisha matano na kukaa juu ya orodha ya wanaoongoza kutikisa nyavu.

Jabir aliyewahi kupita Mtibwa Sugar na kuwepo katika kikosi kilichopanda daraja msimu wa 2023-2024, ametua Polisi Tanzania kufuatia msimu wa 2025-2026 kuitumikia Dodoma Jiji. Akizungumza na Mwanaspoti, Jabir amesema baada ya misimu miwili kutosikika sana, kwa sasa amerejea upya kuhakikisha anaziba mapengo yote na ikiwezekana kutwaa kiatu cha ufungaji bora. Amesema kwa sasa anachofanya ni kuendelea kujifua na kupambana pale anapopata nafasi chini ya kocha wake, Mbwana Makata akieleza kuwa anahitaji historia mpya na kuvunja rekodi za misimu ya nyuma.

“Siwezi kujua mbele kitatokea nini, lakini nahitaji niwe mfungaji bora, nilishafunga mabao mengi ila sijawahi kufikia hatua hiyo, hivyo naendelea kujituma na kupambana kutimiza ndoto.

“Misimu miwili nyuma sikuwa katika kiwango kwakuwa nilishuka hadi Championship nikicheza Mtibwa Sugar niliyopandisha daraja, Dodoma Jiji sikuaminiwa sana kupata nafasi ya kucheza, hivyo naona msimu huu kuwa bora kwangu,” alisema straika huyo.

Kuhusu ubora wake uwanjani, nyota huyo amesema sababu kubwa ni kujituma kuanzia mazoezini na kutimiza malengo kwa kile anachoelekezwa na benchi la ufundi akieleza kuwa anatamani makubwa zaidi.

“Kimsingi lazima wote tupambane kila mmoja kwa nafasi yake tuweze kulinda matokeo haya kwa timu na kumaliza nafasi nzuri kwenye msimamo, lolote linawezekana iwapo tutatimiza wajibu,” alisema.