Amsha amsha za dabi Betika Mtoko wa Kibingwa zilivyonoga Dar
Muktasari:
- Msimu wa tano wa Mtoko wa Kibingwa ulitoa washindi 100, ambayo ni mara mbili zaidi ya washindi wa msimu uliopita waliopata fursa ya kuishuhudia dabi hiyo laivu kwa Mkapa, gharama zote zikilipwa na kampuni ya kubashiri ya Betika.
Zilikuwa siku tatu za kibabe na amsha amsha kwa mashabiki 100 wa Betika Mtoko wa Kibingwa kuanzia Ijumaa hadi jana Jumapili kwenye mchezo wa dabi wa watani wa jadi, Simba na Yanga kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, wale wa Simba wakimaliza dakika 90 kwa kicheko baada ya ushindi wa mabao 2-0.
Mashabiki hao 100 waliokuwa miongoni mwa maelfu waliyoishuhudia dabi hiyo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni washindi wa msimu wa tano wa promosheni ya Mtoko wa Kibingwa kutoka maeneo mbalimbali mbali nchini waliopata fursa ya kuishuhudia dabi hiyo laivu, gharama zote zikiwa za kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betika.
Kabla ya mechi ya jana, washindi kutoka nje ya Dar es Salaam waliwasili Ijumaa na Jumamosi iliyopita kwa ndege na kushiriki katika hafla ya bata la msimu iliyokwenda sanjari na burudani ya muziki iliyoongozwa na msanii maarufu, Christian Bella iliyofanyika Kidimbwi.
Jumapili jana, wakiwa na msafara wa king'ora, mabingwa hao waliishuhudia dabi kwenye uwanja wa Mkapa wakiwa VIP, ikiwa ni muendelezo wa kampuni ya Betika kuwagharamia mabingwa wa promosheni ya Mtoko wa Kibingwa kuishuhudia dabi hiyo hiyo laivu.
Ofisa Habari wa Betika Tanzania, Juvelinaus Rugambwa amesema promosheni hiyo yenye kauli mbiu ya Haina mbambamba imefanyika kwa kiwango bora na washindi kupata matokezi ya nguvu, sanjari na kuishuhudia dabi hiyo kwa hadhi ya pekee huku mashabiki wa Betika Mtoko wa Kibingwa ambao ni wanazi wa Simba wakiwatambia wa Yanga kwa ushindi huo.
Sharifu Nalinga wa Mtwara ambaye ni mnazi wa Simba amesema, bao la pili la Kibu lilimpa furaha mara dufu kwa timu yake hiyo na kuishukuru kampuni ya Betika kwa namna walivyompa fursa ya kuitizama Kariakoo dabi laivu kwa mara ya kwanza.
"Tangu tumefika Dar es Salaam ilikuwa ni furaha kwangu hadi leo (jana) naondoka, Betika imejitofautisha, tumepokelewa kistaa, tumeshiriki bata la msimu na kuwashuhudia laivu watu mbalimbali maarufu ambao awali alikuwa akiwaona kwenye televisheni.
Mnazi mwingine wa Simba, Constantine Mbele wa Ruvuma amese nyota njema ya ushindi huo ilianza kuonekana tangu alipowasili Dar es Salaam juzi Jumamosi.
"Mapokezi tuliyopewa yalinipa amani mno, tukiwa uwanjani tukapata bao la mapema, niliona kabisa Yanga tunawamudu, japo mwanzoni walikuwa wanachonga sana hadi nikaogopa, Kibu alipofunga bao la pili nikajua habari yao imeishia pale, ki ukweli nafuraha mno, nawashukuru zaidi Betika kwa kuleta promosheni ya Mtoko wa Kibingwa ambayo bila hii, labda nisingepata fursa ya kuishuhudia dabi laivu,".
Bakari Kipopele wa Kagera ambaye ni shabiki kindakindaki wa Yanga, aliwapongeza watani zao Simba kwa ushindi akikiri mechi ilikuwa ngumu.