Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amini: Kuna 'sapraizi' ya Dabi ya Kariakoo

AMINI Pict

Muktasari:

  • Amini, ambaye ni shabiki wa Simba, amesema Dabi hiyo ni ngumu kutabiri kutokana na ushindani mkubwa wa timu hizo mbili, lakini akatumia lugha ya utani kueleza kwamba mchezo huo lazima uwe na mshindi au upande mmoja kuumia.

DABI ya Kariakoo inayopigwa kesho, Jumamosi, Oktoba 10, 2026, kati ya Simba na Yanga imeuwasha moto hata kwa mastaa wa muziki, huku mwanamuziki Amini Mwinyimkuu maarufu Amini, akitoa kauli yake kuhusu mchezo huo na kusema kuna upande utatoka na maumivu.

Amini, ambaye ni shabiki wa Simba, amesema Dabi hiyo ni ngumu kutabiri kutokana na ushindani mkubwa wa timu hizo mbili, lakini akatumia lugha ya utani kueleza kwamba mchezo huo lazima uwe na mshindi au upande mmoja kuumia.

“Mchezo ni mgumu. Ila kuna mtu atakufa,” anasema Amini.

Kwa Amini, mapenzi yake kwa Simba si ya msimu mmoja. Mwanamuziki huyo amesema amekuwa akiifuatilia timu hiyo kwa karibu na hata anamiliki jezi za Simba za misimu tofauti, kitu kinachoonyesha ukubwa wa ushabiki wake.


AMI 02

CHAMA MTU

Katika kikosi cha Simba, Amini ana mchezaji anayemkubali zaidi, ambaye ni Chama, anasema kiungo huyo ana akili kubwa ya kucheza mpira na ana uwezo wa kugeuza mchezo wakati wowote.

“Anaweza akakosea hata mara 20, lakini mara ya 21 akakupa furaha. Yule jamaa ana brain kubwa sana ya mpira,” anasema.

Kauli hiyo inaonyesha namna Amini anavyomwamini Chama, ambaye amemuweka pia kwenye nafasi ya namba 10 katika kikosi chake cha Simba kuelekea Dabi hiyo.


AMI 07

HIKI NDO KIKOSI CHA AMINI

Amini amepanga kikosi chake kuanzia langoni akiwa na Tanda Kasali kama namba moja.

Kwenye safu ya ulinzi, amemtaja Shilambo upande wa kulia, Mlingo kushoto, huku Rushen na Atoule wakiwa mabeki wa kati.

Katikati ya uwanja amewaweka Kagoma kama namba sita, Gueye namba saba na Neo Maema namba nane.

Mbele, Mpanzu amepewa nafasi ya namba tisa, Chama akiwa namba 10 na Aoura akikaa kwenye nafasi ya winga/mshambuliaji.

Ni kikosi ambacho Amini anaonekana kukiamini kuelekea mchezo huo mkubwa, huku Chama akiwa miongoni mwa wachezaji anaowapa nafasi ya kufanya tofauti.


AMI 01

WAPYA WAPEWE MUDA

Mbali na Dabi, Amini amezungumzia pia wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba, akiwataka mashabiki wasiwahukumu mapema.

Kwa mtazamo wake, wachezaji wapya wanahitaji muda wa kuzoea mazingira ya klabu, mfumo wa kocha pamoja na wenzao kabla ya kuanza kutoa kiwango chao bora.

Kwa upande wa uongozi wa Simba, Amini ametoa ujumbe mfupi lakini mzito akisisitiza jambo analoliona kuwa muhimu kwa mafanikio ya timu hiyo ni kuwa na umoja wa menejementi nzima ya Simba. "Simba Nguvu Moja,” anasema.