Aliona mwenzake akishinda Bajaj, Balloon yampa yake
USHINDI wa mtu mwingine umekuwa chachu ya mafanikio kwa mjasiriamali Alex Kagesya kutoka mkoani Morogoro ambaye sasa ni mmiliki wa Bajaj mpya baada ya kuibuka mshindi kupitia kampeni ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Kuwa Mchezoni Ushinde.
Safari ya Kagesya kuelekea kwenye ushindi huo ilianza baada ya kushuhudia mkazi mwingine wa Morogoro akikabidhiwa Bajaj aliyoshinda kupitia kampeni hiyo badala ya kuishia kufurahia mafanikio ya mwenzake, tukio hilo lilimpa hamasa ya kujiunga na kampeni hiyo na kujaribu kupata zawadi kama hiyo.
Akielezea namna alivyopata taarifa za kampeni, Kagesya alisema alivutiwa baada ya kuona picha za makabidhiano ya Bajaj kwa mshindi wa kwanza kutoka Morogoro kupitia mitandao ya kijamii.
"Picha hizo zilinifanya kufuatilie zaidi kuhusu kampeni hiyo na michezo inayotolewa na Bahati Nasibu ya Taifa, huku nikitambua kuwa namimj ninaweza kushiriki na kupata nafasi ya kuibuka mshindi," alisema.
Hatimaye, aliamua kuchukua hatua kwa kutembelea tovuti ya www.nationallottery.co.tz na kuchagua mchezo wa BALLOON ambako alishiriki kwa kiasi cha Sh35,000 kabla ya kuibuka mshindi wa Bajaj mpya.
Kwa Kagesya, ushindi huo ni matokeo ya hamasa aliyoipata baada ya kuona mkazi mwenzake akifurahia zawadi yake.
Kilichoanza kama kuvutiwa na picha za makabidhiano kimeishia kwake kupokea ufunguo wa Bajaj na kuingia kwenye orodha ya washindi wa kampeni hiyo.
Ushindi wake unaifanya Morogoro kuendelea kuwa sehemu ya simulizi za mafanikio zinazotokana na kampeni ya Kuwa Mchezoni Ushinde, baada ya mkazi mwingine wa mkoa huo kutangulia kupata Bajaj kupitia kampeni hiyo na hivyo kumtia hamasa Kagesya kushiriki.
Kampeni ya Kuwa Mchezoni Ushinde ilizinduliwa mwezi Mei mwaka huu ikiwa na zawadi mbalimbali zilizolenga kuwapa washiriki nafasi ya kuibuka washindi kupitia michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa.
Katika kipindi cha kampeni hiyo, zawadi za kila siku zilijumuisha simu janja tano, huku zawadi za kila wiki zikiwa Soundbar, Smart TV, Tablets na fedha taslimu kiasi cha Sh1 milioni.
Zawadi nyingine zilizokuwa sehemu ya kampeni hiyo ni pikipiki na Bajaj, ambazo ziliongeza wigo wa zawadi zilizotolewa kwa washiriki waliofanikiwa kuibuka washindi katika vipindi tofauti vya kampeni.
Kupitia zawadi hizo, kampeni hiyo imehusisha washiriki wenye matarajio tofauti, kuanzia wanaolenga kupata vifaa vya kielektroniki na fedha taslimu hadi wale wanaotamani kujinyakulia zawadi kubwa kama pikipiki na Bajaj.
Katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Morogoro, Kagesya alipokea ufunguo wa Bajaj yake kutoka kwa Richard Kimaro, Afisa Masoko wa Bahati Nasibu ya Taifa, ikiwa ni hatua ya kukamilisha safari yake ya ushindi kupitia kampeni hiyo.
Tukio hilo pia linaonyesha namna taarifa za washindi zinavyoweza kuwafikia watu wengine na kuwavutia kufuatilia kampeni zinazotolewa na Bahati Nasibu ya Taifa, kama ilivyokuwa kwa Kagesya ambaye alichochewa na ushindi wa mkazi mwenzake.
Bahati Nasibu ya Taifa inawaalika wananchi wenye umri wa miaka 18 na zaidi kushiriki michezo yake kupitia tovuti ya www.nationallottery.co.tz au kwa kupiga *149*88#, kuchagua mchezo wanaoupenda na kuzingatia masharti ya ushiriki.