Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Akpan mambo magumu Simba, Zoran asema hapanaa

Akpan apewa namba ya Wawa

KIUNGO wa Simba, Victor Akpan huenda akatolewa kwa mkopo kutokana na kushindwa kumshawishi kocha, Zoran Maki ili kumpatia nafasi ya kucheza katika michezo mitatu iliyocheza timu hiyo hadi sasa.

Akpan alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Coastal Union baada ya kuonyesha kiwango bora msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na kombe la Shirikisho (ASFC).

Akpan anacheza nafasi ya kiungo mkabaji ambayo kwenye mechi dhidi ya St George, Yanga na Geita Gold walitumika, Jonas Mkude, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin ambao wawili hawa hawakuwa kwenye pre-season kule Misri.

Inaelezwa kutokana na Akpan kushindwa kumshawishi, Zoran huenda akarudishwa kwa mkopo Coastal Union na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo mpya kutokea Kwara United FC kutokea Ligi Kuu ya Nigeria, Afeez Nosiru.

Mabosi wa Simba inaelezwa wameanza mchakato wa kutafuta kiungo mpya wa ukabaji na Nosiru anapewa nafasi kama chaguo la kwanza ingawa kuna chaguo la pili kama kiungo wa zamani wa Kaizer Chiefs, Teddy Akumu.