Ababa tishio jipya Ligi Kuu Zanzibar
Muktasari:
- Kiungo huyo anayeitwa kwa jina la Abuubak Suleiman Bakari ‘Ababa’ mwenye umri wa miaka 19 ni miongoni mwa wachezaji wenye vitu tofauti hususani akiwa uwanjani anacheza.
MABINGWA wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ msimu wa 2025-2026 imefanya mabadiliko makubwa ya kikosi hicho huku ikivuta kiungo wa kati kutoka kwenye timu yao ya vijana.
Kiungo huyo anayeitwa kwa jina la Abuubak Suleiman Bakari ‘Ababa’ mwenye umri wa miaka 19 ni miongoni mwa wachezaji wenye vitu tofauti hususani akiwa uwanjani anacheza.
Licha ya mwili wake na umri lakini anakitu kikubwa sana ndani yake ikiwa atapatiwa nafasi ya kukuza kipaji chake kwenye timu hiyo iliyomlea.
Mwanaspoti ilipata nafasi ya kumshuhudia akiwa kwenye uwanja wa Mazoezi, Maisara sehemu ambayo KVZ ndipo wanapofanya mazoezi kujiandaa na klabu bingwa pamoja na msimu mpya.
Baada ya kumaliza mazoezi hayo, amesema amefurahishwa na hatua ya kujiunga na timu ya KVZ, akieleza kuwa ni heshima kwake kupata nafasi ya kucheza katika klabu hiyo yenye historia na ushindani katika soka la Zanzibar.
Amee leza kuwa, uhamisho huo unampa hamasa ya kuendelea kuimarisha uwezo wake na kuthibitisha kuwa vijana wanaweza kupata nafasi katika timu kubwa. “Nimekuwa na ndoto ya kucheza katika kiwango cha juu zaidi, nataka kuitumia vizuri nafasi hii kwa kufanya kazi kwa bidii katika mazoezi na kusikiliza maelekezo ya benchi la ufundi,” amesema
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hababuu Ali amesema Ababa ni miongoni mwa wachezaji wenye kiwango bora na kinachovutia.
Hivyo, amesema kutokana na umri alionao anapaswa kulelewa na kawaida vijana wadogo wanatabia ya kufundishika wanapofundishwa.