Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yashusha straika Mrundi

YANGA imefanya sapraizi ya dakika za lala salama za usajili wa Tanzania Bara baada ya kumalizana na straika Mrundi, Fiston Abdulrazak.

Huo unakuwa usajili wa pili wa Kocha Cedrick Kaze raia wa Burundi baada ya kumsainisha Saido Ntibazonkiza ambaye pia ni Mrundi aliyekuwa mchezaji huru. Saido amekuwa staa ndani ya Yanga ambako alipachika penalti ya mwisho iliyowapa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mbele ya watani zo wa jadi Simba.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Yanga, Hersi Said aliwaambia wanachama jana jioni kwenye makao makuu ya klabu hiyo kwamba anashusha jembe ambalo litakidhi haja ya mashabiki wa Yanga kwenye Ligi Kuu Bara ingawa alificha jina lake kabla ya vyanzo vya Mwanaspoti nchini Burundi kulijulisha kwamba anayetua ni Fiston na viongozi wameshamalizana nae kila kitu mpaka mkwanja wake ameshaingiziwa baada ya Kaze kuwahakikishia kwamba jamaa ni mashine.

Fiston anajiunga na Yanga akitokea ENPPI ya Misri ambako alikuwa anavaa jezi namba 12.

Kabla ya hapo amewahi kucheza klabu za Rayon, Sofapaka(Rwanda), Mamelody Sundowns(Sauzi) na De Agosto ya Angola. Mchezaji huyo ana uzoefu na soka la Afrika kwani amecheza pia kwenye nchi za Burundi na Algeria kwa misimu tofauti.

Yanga ambayo haijapoteza mchezo msimu huu, imepania kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali na ndio sababu kubwa ya kufanya usajili hususani kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea mzuguko wa pili wa Ligi Kuu Bara pamoja na kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara lilifungwa jana usiku ambapo klabu mbalimbali zilifanya yao.

Azam wao wamemsajili Mpiana Mozizi, golikipa Mathias Kigonya na wamemchukua kwa mkopo aliyekuwa nyota wao kiungo mshambuliaji Yahya Zayd.

Dodoma Jiji; wao wamemchukua golikipa Manyika Junior, a Kiungo Mshambuliaji Enrick Vitalis Nkosi Kutokea Mwadui na mshambuliaji Mwiba Omary Daga kutoka Biashara United.

Coastal Union; Wamemaliza na kiungo mshambuliaji wa Burundi, Francis Mustafa ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja  akitokea Bugesera ya Rwanda, pia wamemsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Erick Msagati hadi mwisho wa msimu huu, kitasa Pascal Kitenge kutoka AS Nyuki ya DR Congo, Edward Christopher 'Edo',  amesaini mkataba wa miezi sita akitokea Ruvu Shooting, na Ally Ally kutoka KVZ ya Zanzibar.

Namungo; inadaiwa wao wamemrejesha mshambuliaji wao Reliants Lusajo kutoka KMC

Mbeya City: Ally Mustapha 'Bartez',  David Mwasa, Jamal Mwambeleko, Yayo Kato, Toun Jean Didier, Pastory Athanas, Hamis Thabit, Juma Luzio.

Polisi Tanzania: Mshambuliaji Gerald Mathias amejiunga nao akitokea Biashara Utd

Tanzania Prisons: Kenedy Kipepe kutokea Coastal Union, Seleman Mangoma, Shaban William, Stamil Mbonde.