Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Simba wavamia TFF watua na faili zito

Vigogo Simba wavamia TFF

MAMBO yanaonekana kuwa magumu upande wa viongozi wa Simba baada ya jana mabosi wa klabu hiyo kutinga kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanya kikao cha saa 2 ili kumaliza mgogoro uliopo kati yao.

Simba wamekuwa na mzozo mitandaoni na TFF kwenye mambo mawili, wakitaka kujua undani wa mkataba wa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu, GSM na pili kwenye mechi ya watani Barbara Gonzales aliwashutumu kwa kumzuia kuingia eneo la VVIP na familia yake ingawa baadae TFF walifafanua.

Viongozi hao walifika kwenye ofisi hizo wakiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’, Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mangungu pamoja na wanasheria wawili wa klabu hiyo. Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zilisema viongozi hao waliomba kikao na mabosi wa TFF ili kumaliza mambo kwa amani wakiomba mambo mawili makuu kuyamaliza, ufafanuzi wa mkataba wa GSM ambao wanaupinga kwa madai ya kutoshirikishwa, pamoja na kuomba yaishe kwa kitendo Barbara alichokifanya siku ya mechi ya watani wikiendi iliyopita Uwanja wa Mkapa.

Simba waligomea mkataba wa GSM ambao wameingia na TFF wakiwa wadhamini wenza na NBC kwenye Ligi Kuu Bara na kupeleka malalamiko yao FCC ili mkataba huo uchunguzwe .Kuhusu vurugu zilizotokea uwanjani siku ya mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu, Barbara alionekana akimrekodi video ofisa wa TFF (mwanamke) akidai kukataliwa kuingia jukwaa la VVIP akiwa na watoto watatu.

Hata hivyo, TFF ilifafanua kiongozi huyo alikiuka utaratibu wa eneo hilo ambalo haliruhusu kukaliwa na watoto na vile vile watoto hao walikuwa na tiketi ambazo hazikuwa zao.

Imeelezwa kikao hicho kilihusisha pande zote mbili TFF na Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa bodi hiyo Steven Mnguto na Mtendaji Mkuu Almasi Kasongo walikuwepo pamoja na Makamu wa pili wa Rais, Nyamlani pamoja na Mkurugenzi wa sheria wa TFF.

“Walikuja kuomba ufafanuzi wa mkataba wa GSM ingawa hawajafikia mwisho, lakini kuhusu Barbara aliomba msahama lakini suala lake litapelekwa Kamati ya Maadili, kwani Kamati ya saa 72 haiwezi kushughulikia hili suala,” kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.

Mwanaspoti lilipomtafuta Kasongo ili kuzungumzia juu ya kikao hicho na maamuzi yake, alikiri kikao kufanyika lakini na hakuweka wazi majadiliano yao kwani kilikuwa chini ya TFF wao walikuwa wasikilizaji tu.

Aliekeza Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo atafutwe, ingawa alipopokea simu alidai hakuwa na taarifa ya kilichojiri. Hata upande wa viongozi wa Simba waliokwenda kwenye kikao hicho walipotafutwa simu zao za mkononi ziliita pasipo kupokelewa huku mmoja wao akilidokeza Mwanaspoti ilikuwa ni ishu ya siri kati ya pande mbili.


SIMBA 1-0 JKT

BAO pekee la Kibu Denis dhidi ya JKT Tanzania kwenye dakika ya 27 lilitosha kuwatanguliza Simba hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam ndani ya Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wachache jana usiku, Simba ilianzisha sura nyingi mpya na soka lilianza kwa kasi ya kawaida huku wachezaji wa timu zote wakipigiana pasi fupifupi muda mwingi ambazo hazikuwa na madhara zaidi ya kufurahisha mashabiki. Kipindi cha kwanza JKT Tanzania walitawala zaidi kwenye eneo la kiungo kupitia kwa Najimu Benjamin, Japhet Mayungu na Lazaro Constatine ambao walikuwa na maelewano kwenye eneo hilo.

Eneo la Simba kwenye kiungo walikuwa wanacheza Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Ousmane Sakho lakini mara kadhaa walizidiwa ujanja na JKT Tanzania wanaocheza Championship baada ya kushuka daraja msimu uliopita.

JKT walikuwa na mipango ya kuingia ndani kwenye safu ya ulinzi ya Simba lakini umakini wa mabeki Pascal Wawa na Kennedy Juma walikuwa wanapambana nao kuhakikisha hawaruhusu bao huku wakipasiana kwa uzuri na Beno Kakolanya ambaye ni kipa namba mbili wa Mnyama.

Iliwachukua Simba dakika 27 kupata bao baada ya mpira mrefu wa beki Pascal Wawa anayetajwa kuachwa mwezi huu, kumbabatiza beki wa JKT Frank Nchimbi na Kibu akauwahi akawaliza kwa shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Bao hilo liliwaamsha Simba wakitumia haswa upande wa kushoto kwa Peter Banda ambaye

Yusuph Mhilu alishindwa kutumia krosi zake mara kadhaa kuongeza idadi ya mabao.

Upande wa JKT walirudi nyuma na kuanza kucheza soka la kushambulia kwa kushtukiza mbinu ambayo iliwafanya Simba watawale zaidi mpira na kutumia njia ya pembeni kuingia kwenye safu ya ulinzi ya wapinzani wao.

Kipindi cha pili JKT walionekana kuingia na moto wa aina yake na kutokata tamaa kwa kujiamini na kulazimisha mashambulizi lakini walishindwa kupenya ukuta wa Simba ambao waliwazidi kwa uzoefu kwani walijikuta marakadhaa uso kwa uso na Kakolanya lakini wakaishia kupaisha.

Simba walilazimika kufanya mabadiliko mawili ya haraka kipindi cha pili kwa kumuingiza Kapombe na Nyoni ili kuimarisha safu ya kiungo na ulinzi ambapo walionyesha uhai ingawa Simba haikuwa hatari kama ilivyozoweleka. Simba ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Simba: Beno Kakolanya, Israel Patrick/Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Kennedy Juma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Yusuph Mhilu/ Jimmy Mwanuke, Peter Banda, Kibu Denis/Dancun Nyoni na Ousmane Sakho.

JKT Tanzania:John Mwanda, Michael Aidan, Jukumu Kibanda, Frank Nchimbi, Edson Katanga, Richard Maranya, Najimu Benjamin, Lazaro Constatine, Japhet Mayungu, Ramadhan Ibata na Edward Songo.