Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#TBT ZILITRENDI: Mahakama yamtimua kazi Mwakalebela

SIO ZENGWE: Kulalamika serikalini ni kusababisha taharuki?

TAREHE kama ya leo yaani Machi 3, ila ndani ya mwaka 2008 iliripotiwa stori ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF), Fredrick Mwakalebela ni kama hana kazi baada ya mahakama ya kazi kumrejesha katibu mkuu wa zamani wa shirikisho hilo, Ashery Gassabile.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya mahakama hiyo kuridhika kwamba Gassabile aliondolewa TFF kimakosa.
Gassabile aliondolewa kazini mwaka 2006 akiwa katika muda wake wa (probation) wa miezi sita jambo ambalo lilimfanya asiajiriwe hivyo akaamua kukimbilia mahakamani.
Kamati ya Utendaji ya TFF haikuridhika na utendaji kazi wake Gassabile na kuamua kusitisha ajira yake na badala yake akaajiriwa Mwakalebela ambaye siku hiyo ya Machi 3, alikuwa mkoani Manyara kutatua mgogoro wa soka huko.
Habari zilizopatikana siku hiyo zilizema Gassabile ataanza kazi Jumatatu kama Katibu Mkuu wa TFF, lakini shirikisho hilo litakata rufani kupinga uamuzi huo.
Hata hivyo TFF ilisema Mwakalebela ataendelea na kazi zake zote kwa sababu Jumatatu yake wataenda kukata rufaa.
Kwa sasa Mwakalebela ni Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga baada ya kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mei 4, 2019.