Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Migne ashusha Mkenya Yanga

WAKATI mashabiki wa Yanga wakihesabu saa tu kabla ya kumpokea Kocha Mkuu wao, Sebastien Migne, tayari kocha huyo akishirikiana na mabosi wa klabu hiyo wamefanya mambo yao kimya kimya kwa kumshusha Mkenya kambini.

Mabosi hao wa Jangwani wamemshusha kimyakimya kocha wa makipa kutoka Kenya, Razack Ssiwa ambaye sasa atakuwa na kazi ya kuwapandisha viwango makipa wa timu hiyo baada ya Migne kumpitisha kuungana na Juma Mwambusi anayeendelea kuinoa timu yangu Cedric Kaze atimuliwe.

Ssiwa sio mgeni ndani ya Yanga kwani amewahi kufanya kazi mara kadhaa ndani ya timu hiyo na sasa amerejeshwa baada ya Migne kumpitisha wakati akiwa njiani kuja kuungana nao kambini.

Kocha huyo Mkenya ndiye aliyempa tuzo mbili za Kipa Bora, Faruk Shikhalo aliyeko Jangwani wakati wakifanya kazi wote ndani ya timu ya Bandari FC ya Kenya hatua ambayo iliwavutia Yanga na kumsajili misimu miwili iliyopita.

Mkenya huyo ametua Yanga kuchukua nafasi ya Vladimir Niyonkuru aliyefurushwa sambamba na Kaze pamoja na aliyekuwa kocha msaidizi, Nizar Khalfan kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo na Taifa Stars.

Yanga inajiandaa na mchezo wao wa Kombe la ASFC dhidi ya Tanzania Prisons mechi itakayopigwa Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumatano ya April 7 baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzisogeza mbele mechi zote za Raundi ya 16 Bora kutokana na uwepo wa maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli kilichotokea Machi 17 na kuzikwa juzi kijijini kwao Mlimani, Chato.