Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chuga aitwa na vigogo Brazil kwa majaribio

Muktasari:

  • Palmeiras ni miongoni mwa timu zenye heshima kubwa Brazil kwani imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo mara 12.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Issa Abushiri 'Chuga Boy' amepata fursa ya kufanya majaribio katika klabu ya Palmeiras inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil.

Palmeiras ni miongoni mwa timu zenye heshima kubwa Brazil kwani imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo mara 12.

Hilo limethibitishwa leo Jumatano, Novemba 18, 2026 na Rais wa Yanga, Hersi Said katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani, Dar es Salaam.

“Pamoja na kuwapa nafasi vijana ndani ya timu yetu, tumekuwa tukifungua milango ya fursa za kimataifa kwa wachezaji wenye vipaji ili waweze kupata uzoefu na kuendeleza taaluma zao katika mazingira makubwa zaidi ya soka.

"Miongoni mwa wachezaji hao ni Abushiri 'Chuga', ambaye tayari tumeanza kupokea ofa na maombi kutoka katika baadhi ya klabu na taasisi za soka za kimataifa zinazotaka kumpa nafasi ya kufanya majaribio.

"Kwa sasa tupo katika hatua nzuri za kukamilisha taratibu za kumwezesha kwenda nchini Brazil kufanya majaribio katika klabu ya Palmeiras, ambayo ni miongoni mwa klabu kubwa na zenye historia nzuri katika soka la Brazil.

"Klabu hiyo imeonyesha nia ya kumpa fursa Abushiri, na kwa sasa tunaendelea na taratibu za nyaraka zake, ikiwemo maandalizi ya visa. Tunasubiri pia arejee kutoka katika majukumu ya timu ya taifa ili tuweze kukamilisha hatua zinazofuata na kumruhusu kwenda kufanya majaribio hayo," amesema Hersi.

Hersi amesema kuwa klabu hiyo inaamini kwamba kuuza wachezaji ni miongoni mwa fursa za kuiimarisha kiuchumi.

"Pamoja na changamoto hizo, klabu imeendelea kutekeleza majukumu yake na kutumia fursa mbalimbali za kimichezo na kibiashara kwa manufaa ya taasisi yetu.

"Miongoni mwa hatua tulizozichukua ni kutoa fursa kwa baadhi ya wachezaji wetu kujiunga na klabu mbalimbali kupitia mfumo wa uhamisho wa wachezaji.

"Hatua hii imekuwa na manufaa mawili makubwa: kwanza, kuisaidia klabu kupata mapato yatakayochangia katika uendeshaji wake na pili, kuwapa wachezaji wetu fursa ya kukutana na changamoto mpya, kupata uzoefu zaidi na kuendeleza taaluma zao za soka," amesema Hersi.