Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zolla afagilia ‘mafaza’ Championship

ZOLLA Pict

Muktasari:

  • Rhino ni mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2025-2026, baada ya kuifunga Bandari Tanzania iliyopanda kwa kuongoza kundi A na pointi 32 kwa penalti 4-2 baada ya sare ya kufungana mabao 2-2, mechi iliyopigwa Juni 17, 2026.

KIUNGO mkabaji na nahodha wa Rhino Rangers ya Tabora, Ntilla Zolla Hussein amesema ongezeko la wachezaji mafaza katika Ligi ya Championship ni sababu inayochangia ushindani kwa kila timu inayoshiriki, jambo linalozidi kuvutia kila msimu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Zolla aliyewahi kutamba na timu mbalimbali zikiwemo za, JKT Kanembwa na Mashujaa FC zote za mjini, Kigoma, amesema ongezeko la wachezaji wakubwa na wazoefu umeongeza chachu ya ushindani na vita ya kupanda daraja.

“Championship ya misimu mitano nyuma na sasa ni tofauti kwa sababu kumekuwa na wimbi kubwa la wachezaji wanaotoka hadi Ligi Kuu Bara wanaoshuka kucheza daraja la chini, hii inaonyesha ushindani ni mkubwa ikiwa hautajipanga,” amesema Zolla.

Aidha, Zolla amesema licha ya ushindani mkubwa ila watahakikisha wanaipigania timu hiyo irejee tena Ligi Kuu Bara, baada ya kusota kwa muda mrefu, tangu iliposhuka daraja msimu wa 2013-2014, ilipomaliza mkiani mwa nafasi ya 14 na pointi 16.

Rhino ni mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2025-2026, baada ya kuifunga Bandari Tanzania iliyopanda kwa kuongoza kundi A na pointi 32 kwa penalti 4-2 baada ya sare ya kufungana mabao 2-2, mechi iliyopigwa Juni 17, 2026.