Mwalwisi afichua jambo IAA SC
Muktasari:
- Timu ya IAA SC ya Arusha ilifuzu kucheza Ligi ya Championship kwa msimu wa 2026-2027, kupitia mechi ya ‘Play-Off’, baada ya kuitoa African Sports ya Tanga kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda nyumbani 2-1, kisha ugenini ikatoka sare ya bao 1-1.
KOCHA Mkuu wa IAA SC, Maka Mwalwisi amesema licha ya ugeni wa kikosi hicho kushiriki Ligi ya Championship msimu wa 2026- 2027, kwa mara ya kwanza, ila sio kigezo cha wao kufanya vibaya, kwa sababu wana wachezaji bora na wenye uzoefu mkubwa.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mwalwisi aliyejiunga na IAA SC ya jijini, Arusha akitokea Mbeya Kwanza yenye maskani mjini, Tabora, amesema wachezaji wanaounda kikosi hicho ni wazoefu na mashindano hayo, jambo walilozingatia katika usajili wao.
“Baada ya kupata ofa ya kuifundisha, jambo nililowaambia wahakikishe tunapata wachezaji wazoefu wa Ligi ya Championship, nashukuru walinishirikisha katika machaguo yangu na nikawapendekeza wale watakaotusaidia msimu huu,” amesema Mwalwisi.
Kocha huyo aliyezifundisha Ihefu kwa sasa Singida Black Stars na TMA FC iliyokuwa Arusha kisha kuhamishia makazi yake mjini, Iringa, amesema anahitaji muda zaidi wa kutengeneza kikosi cha ushindani, kwa sababu wachezaji wengi ni wapya.
IAA SC inayoshiriki Ligi ya Championship msimu wa 2026-2027, kwa mara ya kwanza, kabla ya mechi ya jana Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar, imecheza minne, ikishinda moja, ikitoka sare moja na kupoteza mbili, ikiwa nafasi ya 10 na pointi nne.
Timu ya IAA SC ya Arusha ilifuzu kucheza Ligi ya Championship kwa msimu wa 2026-2027, kupitia mechi ya ‘Play-Off’, baada ya kuitoa African Sports ya Tanga kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda nyumbani 2-1, kisha ugenini ikatoka sare ya bao 1-1.