Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zimevuja... Jezi zitakazotumika EPL msimu ujao

JEZI Pict

Muktasari:

  • Msimu ujao wa EPL unatarajiwa kuanza rasmi Agosti 15, mwaka huu ambapo timu kibao zitakuwa zinaangalia uwezekano wa kuinyang’anya taji Liverpool ambayo ndio bingwa wa sasa.

LONDON, ENGLAND: WAKATI maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England yakiendelea baadhi ya timu tayari zimeshatambulisha jezi mpya huku nyingine zikivuja.

Msimu ujao wa EPL unatarajiwa kuanza rasmi Agosti 15, mwaka huu ambapo timu kibao zitakuwa zinaangalia uwezekano wa kuinyang’anya taji Liverpool ambayo ndio bingwa wa sasa.

Hapa tumekuletea muonekano na maelezo ya jezi zote zilizotambulishwa na kuvuja hadi sasa.

JEZ 05

ARSENAL

The Gunners tayari wamezindua jezi yao ya nyumbani kwa msimu ujao. Jezi hiyo ya rangi nyekundu ina mapambo meupe pamoja na chapa ya herufi “A” ya kigozi iliyochanganywa ndani ya sehemu ya mbele ya jezi.

Tofauti na jezi za nyumbani za Arsenal za miaka ya hivi karibuni, jezi mpya, bukta na soksi vina rangi nyekundu na nyeupe tu, bila rangi ya bluu au dhahabu.

Ingawa jezi za pili na za tatu za klabu bado hazijatolewa rasmi, baadhi ya mashabiki wamezivujisha mtandaoni.

Jezi ya ugenini ya Arsenal inayodaiwa inafanana na jezi yao ya tatu ya msimu wa 2021-22 ilisambaa mitandaoni. Jezi hiyo ilionekana kuwa na rangi ya bluu iliyokoza na bluu isiyokoza, pia ina nembo ya Gunners yenye rangi nyeupe.

Pia kuna mapambo mekundu pembeni.

Jezi ya tatu iliyovuja ina mchanganyiko wa jezi namba tatu za msimu wa 2008-09 na 2009-10.

Jezi ni nyeupe ikiwa na nembo ya kanoni na nembo ya Adidas ya rangi ya maruni, pamoja na mapambo ya dhahabu kwenye kola na mikono, pia ina mstari wa alama maarufu za Adidas mabegani pia ni wa rangi ya maroon.

JEZ 02

CHELSEA

Jezi mpya ya Chelsea inafanana kwa kiasi kikubwa na ile ya msimu wa uliopita. Ni ya rangi ya bluu.

Jezi ya ugenini pia inafanana na ya msimu uliopita. Jezi mpya ya ugenini ya Chelsea ina rangi ya nyeupe kama ya zamani lakini ina mistari minane midogo  ya bluu na ya rangi nyekundu katikati.

Pia ina mapambo mekundu na meusi kwenye kingo za mikono. Utofauti ni kwamba hakuna nembo yao ya kung’aa.

JEZ 08

LIVERPOOL

Kuanzia msimu wa 2025-26, Adidas atakuwa msambazaji wa jezi za Liverpool, akichukua nafasi ya Nike.

Adidas hapo awali aliwahi kushirikiana na Liverpool kuanzia mwaka 1985 hadi 1996 na tena 2006 hadi 2012.

Jezi mpya ya nyumbani ya Liverpool inafanana sana na ile ya msimu wa 2010-11 ikiwa na muundo wa  rangi nyekundu na nyeupe.

Ikiwa na mistari mitatu maarufu ya Adidas mabegani na mstari mwembamba mweupe kila upande, jezi mpya ya ugenini ya timu hiyo ni nyeupe yenye mapambo mekundu.

Kuna tofauti kubwa pia kwenye nembo ya Liverpool katika jezi namba tatu ambayo katika kukumbushia enzi za miaka ya 1980, jezi ya tatu inatumia nembo ya zamani  iliyotambulishwa miaka 38 iliyopita.

Nembo hiyo ilianzishwa mwaka 1987 na ilitumika kwa miaka mitano hadi 1992, mwaka wa maadhimisho ya miaka 100 ya Liverpool.

Sasa inatumika kwenye jezi ya tatu ya timu kwa msimu wa 2025-26.

Jezi hiyo mpya ni ya kijani ikiwa ina mistari iliyofifia mbele. Pia inatumia nembo ya Adidas Original kwenye kifua.

JEZ 06

MANCHESTER CITY

Manchester City wamechagua urahisi katika jezi yao ya nyumbani ya msimu wa 2025-26.

Jezi hiyo ina vipengele vya rangi nyeupe ikiwamo mstari unaofanana na mkanda upande wa mbele.

Hata hivyo, jezi za ugenini na zile namba tatu zinadaiwa zimetofautiana sana na hii jezi ya nyumbani.

Jezi ya ugenini ina rangi nyeupe na michoro ya mashabiki wa Man City wakishangilia kwa staili yao ya  “poznan” (ushangiliaji wa pamoja wa kugeuka nyuma kuangalia mbali na uwanja, wakiwa wamekumbatiana mabega na kuruka-ruka kwa pamoja), pamoja na mstari mweusi na mwekundu unaopita mbele ya jezi.

Etihad Airways, mdhamini wa klabu, amewekwa chini ya nembo ya timu badala ya katikati ya jezi.

Kwenye upande wa jezi namba tatu zinazodaiwa kuwa vimevuja, zipo za aina mbili. Ya kwanza ina rangi ya machungwa ang’avu ikiwa na mstari wa rangi nyeusi na dhahabu.

Ya pili ni tofauti kabisa na jezi yoyote iliyowahi kutumiwa kwenye Ligi Kuu.

Jezi hiyo ya kijivu ina muundo wa matone ya mvua na nembo ya Man City katikati juu ya nembo ya Puma.

Pia ina mapambo ya kijani ang’avu.

JEZ 07

MANCHESTER UNITED

Manchester United bado hawajazindua jezi yao ya nyumbani kwa msimu wa 2025-26.

Hata hivyo, picha ya jezi hiyo imevuja mtandaoni.

Jezi hiyo mpya inayodaiwa kuwa ni ya nyumbani ya Man United inafanana sana na ile ya msimu wa 2023-24 ikiwa na mistari ya Adidas ya rangi nyeusi mabegani.

Jezi hiyo nyekundu pia inaonekana kuwa na mchoro unaopita kwenye mikono.

Picha ya jezi ya golikipa wa Man Utd pia imevuja mtandaoni wiki za hivi karibuni.

Jezi hiyo ya kijani ina mapambo meupe pamoja na nembo ya Adidas.

Jezi ya ugenini inayodaiwa kuwa ni ya Man Utd ambayo pia imevuja ni nyeupe. jezi namba tatu ni ya bluu iliyokoza ikiwa na maandishi na mapambo ya njano.

JEZ 03

NEWCASTLE

Newcastle wamezingatia utamaduni wao kwenye jezi yao ya nyumbani ya 2025-26.

Kama kawaida, jezi ina mistari ya rangi nyeusi na nyeupe iliyosimama.

Lakini kuna mabadiliko madogo, rangi ya bluu isiyokoza imeongezwa kwenye toleo hili jipya.

Mistari hiyo ya bluu nyepesi inaizunguka kola, pembeni mwa jezi na kwenye kingo za mikono.

JEZ 01

NOTTINGHAM FOREST

Jezi ya nyumbani ya Nottingham Forest iliyovuja ina mwonekano wa zamani ikiwa na mistari yenye umbo jembamba ya rangi nyeupe.

Pia ina kola, ambayo haijaonekana kwenye jezi ya Forest tangu mwaka 2012.

Jezi ya ugenini ambayo pia imevuja ni nyeupe ikiwa na mistari ya Adidas ya kijivu mabegani.

Pia ina mchoro uliounganishwa kwenye sehemu ya mbele ya jezi.

JEZ 04

TOTTENHAM

Washindi hawa wa Europa League, wamezindua jezi yao ya nyumbani ya msimu wa 2025-26 wiki hii.

Jezi hiyo mpya ni tofauti sana na mitindo ambayo Spurs wamekuwa wakitumia miaka ya hivi karibuni.

Nembo ya Spurs pia imewekwa katikati ya jezi, juu ya nembo ya Nike.

Wakati huohuo, jezi ya ugenini ya Tottenham ina rangi nyeusi na mistari hafifu inayopita kwa usawa na wima mbele ya jezi na kwenye bukta, ikitengeneza muundo wa kisanduku.