Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga inamhitaji Shalulile wa 2021/2023

SHALULILE Pict

Muktasari:

  • Huyu ni mshambuliaji mwenye historia nzuri ya kufunga mabao katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini lakini mtazamo wa kijiwe ni kwamba Yanga inahitaji jamaa awe na fomu itakayompa makali aliyokuwa nayo kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 na asiwe wa misimu miwili iliyopita.

Kijiwe kwa sasa kimetawaliwa na kelele za tambo kutoka kwa mashabiki wa Yanga baada ya kumnasa mshambuliaji Peter Shalulile, raia wa Namibia ambaye sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Mamelodi Sundowns.

Huyu ni mshambuliaji mwenye historia nzuri ya kufunga mabao katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini lakini mtazamo wa kijiwe ni Yanga inahitaji jamaa awe na fomu itakayompa makali aliyokuwa nayo kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 na asiwe wa misimu miwili iliyopita.

Fomu hiyo pamoja na ubora wa Shalulile, ilichangiwa pia na ufiti wa hali ya juu ambao alikuwa nao tofauti na hivi karibuni na majeraha yalikuwa yakimsumbua.

Misimu ya 2021/2022 na 2022/2023, Shalulile alikuwa wa moto sana katika kufumania nyavu kuanzia katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini hadi katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika msimu wa 2021/2022, Shalulile alipachika mabao 23 katika mechi 30 za Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) huku mabao matatu akifunga katika mechi nane za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimu wa 2022/2023, aliweka mpira kambani mara 12 katika mechi 21 za PSL na katika Ligi ya Mabingwa Afrika alipachika mabao sita katika mechi nane.

Hata hivyo mambo hayakuwa mazuri kwake katika misimu miwili iliyopita ambapo hakupata nafasi kubwa ya kucheza kutokana na kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyolilazimisha benchi la ufundi la Mamelodi Sundowns kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.

Kumbukumbu zinaonyesha msimu uliopita, jamaa alifunga mabao matatu katika mechi 13 za Ligi Kuu ya Sauzi na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akifunga mabao mawili katika mechi tano na katika msimu wa 2024/2025, alifunga mabao sita katika mechi 24 za ligi ya nyumbani huku katika mechi 12 za Ligi ya Mabingwa Afrika akifumania nyavu mara tatu.

Kuhusu umri wa miaka 32 ambao Shalulile anao, siyo jambo la kuliwekea maanani sana kwa vile umri ni namba tu. Wapo wenye umri mkubwa waliofanya vizuri na wapo wenye umri mdogo waliochemsha.