Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazanzibar wananikumbusha Wabrazil na majina yao ya utani

JICHO Pict


NCHI ina mambo mengi. Wakati mwingine tusiongee mambo mengi ya msingi. Tunaweza kujiuliza mambo ya kawaida tu ambayo inawezekana hayana msingi lakini yanaweza kutufanya tutabasamu na kupoteza muda.


Kwa mfano. Hivi Wazanzibar huwa wanatoa wapi majina ya utani ya kupachikwa ‘Nicknames’. Huwa wananifanya niwe na tabasamu usoni. Huwa ni kama Wabrazil tu. Majuzi Yanga walianza kumtumia mchezaji kutoka Zanzibar. Anaitwa Casemiro.


Jina lake halisi? Kumbe ni Abdulnasir Mohamed Abdallah. Alipataje jina la Casemiro? Hatujui. Lakini kwa nini tushangae. Wazanzibar ni mabingwa wa majina haya. Hawana tofauti sana na Wabrazil.

Wametuletea kijana ambaye anasumbua mpira wetu. Anaitwa Fei Toto. Jina lake halisi? Anaitwa Feisal Salum Abdallah. Wapi limepatikana jina la Fei Toto? Sio uwanjani. Siku moja Fei alitusimulia akatuambia jina limepatikana kwa bibi yake.

Kwamba bibi alikuwa anakatisha jina la Feisal akamuita Fei. Na kwa sababu alikuwa mtoto akawa anamuita ‘Fei Toto’.  Ina maana jina hili lilitokea mtaani tu. Kabla Fei hajaanza mpira. Kumbe kuna majina yao yanaanzia nyumbani katika familia na mengine yanaanzia wakati wanacheza soka.

Haya yanayoanzia katika kucheza soka kama Casemiro inawezekana ndiyo mambo ambayo yalimkuta Nadir Haroub. Wote tulimfahamu kwa jina la Cannavaro. Hii haishangazi sana. Kama ilivyokuwa kwa Casemiro basi ndivyo ambavyo ilianzia kwa Cannavaro.

Kulikuwa na Abdi Kassim ‘Babi’. Hili hatuwezi kujua lilitoka wapi. Labda lilitoka mtaani kama ilivyokuwa kwa Fei Toto kwa sababu hatujawahi kusikia kama kuliwahi kuwa na mchezaji ambaye aliwahi kuitwa Babi. Labda pia hili la Babi lilitokana na jina la Abdi kwa sababu kuna mlinganisho.

Kuna Masoud Nassor alicheza Simba. Jina lake maarufu lilikuwa Cholo. Wazanzibar wengi ambao wanaitwa Nassoro huwa wana jina la utani la Cholo. Sio jambo la kushangaza sana. Hata sasa hivi kuna mchezaji anacheza ligi kuu ya Bara akiwa anatokea Zanzibar huwa anaitwa Cholo. Jina lake ni Nassoro.

JICH 01

Wapo wengi lakini zamani walikuwa wengi zaidi katika zama za mpira ule. Wengine naweza kuwasahau lakini kulikuwa na akina Nassoro Mwinyi ‘Bwanga’. Itashangaza kidogo lakini zamani watu waliokuwa wanavaa suruali pana, hasa ambayo ilikuwa inatanuka maeneo ya chini tulikuwa tunaita bwanga.

Kulikuwa na Said Seif ‘Kibichwa’. Hili lazima litakuwa jina la mtaani tu. Sitaki kuongea zaidi kuhusu mtazamiko wa Kichwa chake au inawezekana alikuwa na tabia ya kuzidisha chenga nyingi na kuvimba Kichwa wakati akiwa na mpira.

Rafiki yangu, kipa namba moja wa Zanzibar wakati huo, Ally Bushir alikuwa anaitwa George Bush. Nadhani Wazanzibar walikuwa wanakatiza jina lake kutoka Bushiri kwenda kwa Bush. Alikuwa kipa mahiri.

Miezi kadhaa iliyopita alifariki mmoja kati ya viungo wazuri waliowahi kutokea katika historia ya Zanzibar. Ally Sharrif ‘Aldoph’. Naambiwa kwamba huyu alipewa jina hilo kutokana na kulinganishwa na staa wa zamani wa soka la Tanzania bara, Aldoph Rishards.

Waliwahi kuwa na mchezaji aliyeitwa Ubwa Makame ‘Mzungu’. Lakini huyu pia alikuwa anafahamika kwa jina la ‘Mr Freekick’. Huyu alitupa majina mawili ya asili tofauti. Mzungu lilitokana na rangi yake au tabia yake. Hili la ‘Mr Freekick’ lilitokana na uhodari wake katika kupiga mipira ya adhabu.

Hawa ni wachezaji wachache sana wa Zanzibar ambao nimewakumbuka kutoka Zanzibar lakini nafahamu kuna wachezaji wengi mahiri wa Zanzibar ambao wana majina ya utani. Inaanzia mtaani hadi katika mpira.

JICH 02

Huku bara kuna wachezaji wengi mahiri ambao wangeweza kupewa majina mengi ya utani lakini inaonekana sio utamaduni wetu. Kwa mfano Mrisho Ngassa. Aliendelea kuwa Mrisho Ngassa mpaka leo.

Edibily Lunyamila aliendelea kuwa yule yule tu. Simon Msuva, Thomas Ulimwengu, Clement Mzize na wengineo kibao hawana majina ya utani. Wapo ambao wamepewa majina ya utani lakini hayajawakaa sana na inaonekana kama vile tunawalazimisha.

Kwa mfano, Mbwana Samatta huwa tunamuita ‘Samagoal’, lakini sio jina lililomkaa sana kama Fei Toto. Aishi Manula tunamuita ‘Air Manula’ lakini sio jina ambalo tunaweza kumuita moja kwa moja kama ambavyo wachezaji wa Zanzibar yanavyokuja moja kwa moja.

Wazanzibar wananikumbusha Wabrazil na majina yao ya utani. Ni wachezaji wachache wa Brazil ambao hawana majina ya utani. Karibu kila mmoja ana jina la utani. Jina la mzaha. Nitchoka kueleza walipataje majina yao lakini mengi ni utani au mzaha. Wabrazil wanakuwa na majina marefu halafu linatokea jina moja tu la utani. Sio jina lake wala sio la familia. Mfano ni Jose Roberto Gama de Oliveira. Walimuita Bebeto. Kuna Edson Arantes do Nascimento. Wenyewe walimuita Pele.

Nelson de Jesus Silva. Wenyewe walimuita Dida.