Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita usiku mdogo wa Ulaya inaanza

UEFA Pict

Muktasari:

  • Kabla ya kuanza kwa Europa League msimu huu kuna utabiri umefanyika wa nani atapenya na au kubeba ndoo hiyo. Lakini ni timu gani imeshinda mashindano hayo mara nyingi zaidi?

LONDON, ENGLAND: LEO, Ligi ya Europa msimu 2026-27 inaanza ambapo timu mbalimbali zitakuwa viwanjani, huku ikitarajia kuendelea pia kesho.

Kabla ya kuanza kwa Europa League msimu huu kuna utabiri umefanyika wa nani atapenya na au kubeba ndoo hiyo. Lakini ni timu gani imeshinda mashindano hayo mara nyingi zaidi?

Europa League inaanza huku timu 36 zikiwa tayari kwa hatua ya ligi yenye siku nane za mechi, itakayoanza Jumatano usiku hadi katikati ya Januari. Mwishoni mwa michezo hiyo, timu zitawekwa katika msimamo mmoja mkubwa, ambapo nane za juu zitasonga moja kwa moja hatua ya 16 bora, huku zitakazomaliza nafasi ya tisa hadi ya 24 zikicheza hatua ya mchujo ili pia kufuzu hatua ya mtoano.

Kuanzia hapo, mfumo utakuwa wa mtoano wa moja kwa moja hadi kubaki timu mbili zitakazocheza fainali katika Uwanja wa Waldstadion, Frankfurt, Ujerumani, Mei 26, 2027. Msimu uliopita, Aston Villa ilitwaa kombe hilo, lakini mafanikio yao yalimaanisha kwamba walifuzu moja kwa moja kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Hivyo, kwa mara nyingine tena, kutakuwa na mshindi tofauti wa Europa League msimu huu.

England msimu huu ina Bournemouth, Sunderland na Crystal Palace, inaweza kujiamini baada ya mafanikio ya Villa, huku Tottenham ikiwa ilishinda Europa League mwaka uliotangulia. Hii ina maana kwamba kumekuwa na washindi kutoka England katika mashindano hayo kwa misimu miwili mfululizo. Kabla ya mashindano ya msimu uliopita ilitabiriwa kwamba Villa ingetwaa ubingwa kabla hata mpira haujachezwa. Na safari hii, kuna timu nyingine ya Ligi ya Kuu England inapewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa.


UE 02

WANAOPEWA NAFASI KUBWA KUSHINDA

Katika msimu wa kwanza kushiriki mashindano ya Ulaya, Bournemouth ndiyo inayopewa nafasi kubwa zaidi ya kwenda mbali na kushinda Europa League 2026-27. Kulikuwa na maswali kadhaa kuhusu timu hiyo baada ya mabadiliko mengine makubwa yaliyotokea wakati wa kiangazi, safari hii kocha Andoni Iraola akiondoka kwenda Liverpool na beki muhimu wa kati, Marcos Senesi, kuondoka kwa uhamisho huru kwenda Spurs.

Hata hivyo, wameanza vizuri chini ya Marco Rose, na wanapewa nafasi ya kuendelea kuwa imara msimu mzima wakipewa nafasi ya ya asilimia 14.3 ya kubeba ubingwa kuliko timu nyingine yoyote. Bournemouth pia inamaliza juu ya msimamo wa hatua ya ligi hiyo kwa asilimia 15.1 kuliko timu nyingine yoyote. Hata hivyo, wana ushindani mkubwa, huku kukiwa na timu moja iliyo karibu sana nao katika kuwania nafasi ya kuwa kinara, na timu nyingine tano ambazo haziko mbali sana katika matumaini ya kushinda mashindano hayo.

Benfica iko nyuma kidogo tu ya Bournemouth, ikishinda Europa League katika asilimia 14.0. Mabingwa hao mara nyingi wa Ureno ambao msimu uliopita walikuwa chini ya Jose Mourinho walimaliza nafasi ya tatu katika Primeira Liga, lakini sasa wanaongozwa na kocha mwingine anayefahamika kwa klabu za England aliyekuwa kocha wa Fulham, Marco Silva.

Benfica imeshinda michezo mitano na kutoka sare moja katika michezo sita ya ligi msimu huu, ikiwa imefunga mabao mengi zaidi (21) kuliko timu nyingine yoyote. Katika ligi 10 bora za Ulaya, ni Slavia Prague (23) na PSV (22) pekee zilizofunga mabao mengi zaidi. Kwa sasa Benfica iko nafasi moja tu chini ya Bournemouth katika timu zinazotabiriwa kubeba Europa League.

Inayofuata kama timu ya tatu kupewa nafasi kubwa ya kushinda Europa League ni Bayer Leverkusen, ambayo imerejea kwenye mashindano  baada ya 2025-26 iliyokuwa ya kukatisha tamaa, ambapo ilimaliza nafasi ya sita Bundesliga, miaka miwili tu baada ya kushinda ubingwa bila kupoteza mchezo wowote msimu mzima chini ya Xabi Alonso.

Sasa ikiwa chini ya kocha ambaye hana uzoefu mkubwa, aliyekuwa kocha wa Toulouse, Carles Martínez Novell, Leverkusen ni timu isiyotabirika zaidi kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma; ikipoteza mchezo wa kwanza wa msimu dhidi ya Elversberg, timu mpya katika Bundesliga, ni mfano wa hilo. Hata hivyo inaaminika kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda Europa League ikipewa asilimia 10.2.

Union Saint-Gilloise kwa mshangao iko nafasi ya juu kiasi ikipewa asilimia 8.6 kubeba ubingwa, ambapo washindi hao wa pili wa Ligi Kuu Ubelgiji (Belgian Pro League) msimu uliopita walishiriki hatua za kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu huu wa kiangazi, lakini waliondolewa kwa tofauti ndogo na Bodo/Glimt, hivyo wameishia Europa League. Tayari wameanza msimu wa ndani kwa kuvutia na watatoa upinzani mkali kwa timu yoyote watakayokutana nayo, hata kama jina lao halina uzito mkubwa miongoni mwa timu nyingine kwenye mashindano hayo.

Sunderland, ambayo imerejea Ulaya kwa mara ya pili katika historia yake baada ya kushiriki Cup Winners’ Cup msimu wa 1973-74, inaweza kuwa miongoni mwa timu zinazowania ubingwa wa Ulaya. Katika msimu wao mwingine pekee wa kushiriki mashindano ya Ulaya walishinda mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa kwa mechi mbili, lakini wakaondolewa na Sporting CP katika raundi ya pili. Safari hii watacheza angalau mara mbili ya michezo waliyocheza wakati huo (michezo minane), lakini watakuwa na matumaini ya kwenda mbali katika mashindano. Wanapewa asilimia 82.3 ya kufika hatua ya 16 bora, na asilimia 8.3 ya kwenda hadi mwisho na kushinda mashindano.

Hilo kwa kiasi kikubwa linatokana na kampeni yao iliyokuwa ya kuvutia msimu uliopita, lakini wakati huo hawakulazimika kusimamia ratiba za mashindano ya ndani na Ulaya kwa wakati mmoja. Hilo ni jambo ambalo hawajawahi kulazimika kulifanya kwa kiwango bora, hivyo itakuwa jambo la kuvutia kuona watakavyofanya.


UE 01

TIMU NYINGINE ZINAZOWANIA NDOO

Juventus inapewa asilimia 7.8 ya kubeba ubingwa, lakini licha ya kuwa klabu kubwa yenye historia kubwa katika hatua hii ikiwa imeshinda UEFA Cup mara tatu, Kombe la Washindi Ulaya mara moja na Kombe la Ulaya/Ligi ya Mabingwa mara mbili, mafanikio ya hivi karibuni Ulaya yalikuwa msimu wa 1995-96.

Juventus ni moja ya vigogo waliopoteza makali, na mashindano hayo yanawapa nafasi nzuri ya kurejea kwenye njia ya ushindi.

Crystal Palace inafuata katika mfululizo wa timu zinazopewa nafasi ikiwa na asilimia 7.3 ya kushinda Europa League. Ghafla imejenga historia katika mashindano ya Ulaya baada ya kushinda Conference League katika msimu wake wa kwanza kushiriki mashindano ya Ulaya uliopita.

Inafuata AC Milan inayopewa asilimia 5.3 na haiwezi kuondolewa katika orodha ya wanaowania ubingwa, huku Rennes (asilimia 3.9), Lyon (asilimia 3.2) na Hoffenheim (asilimia 2.3) zikikamilisha orodha ya timu zenye nafasi ya zaidi ya asilimia mbili ya kushinda mashindano.


ZINAOPEWA NAFASI NDOGO SANA

Msimu wa Europa League 2026-27, timu mbili kati ya 36 zilizoshiriki zilishindwa kushinda mashindano hayo hata mara moja; Torreense ya Ureno na OFI Crete ya Ugiriki. Kwa mtazamo, timu hizo zina nafasi ndogo ya kushinda Europa League.

Vilevile ipo Ararat-Armenia ya Armenia inayopewa asilimia 0.01 ya kutwaa ubingwa, huku Celje ya Slovenia, Lillestrom ya Norway na Hapoel Be’er Sheva ya Israel zikipeaa asilimia 0.06, na NEC ya Uholanzi asilimia 0.2.