Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya Championship inavyoanza upyaa

CHAMPIONSHIP Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, wadau wa soka nchini wamesema licha ya timu hizo tatu kupewa nafasi kubwa, zipo nyingine zinazoweza kushangaza kutokana na malengo na mipango yao ndani na nje ya uwanja, huku wakieleza matarajio yao ya ligi yenye ushindani mkubwa.

WAKATI Ligi ya Championship msimu wa 2026-2027 ikitarajiwa kuanza Ijumaa, Septemba 11, 2026, timu tatu zinapewa kipaumbele cha kupanda Ligi Kuu kutokana na uzoefu, historia na nguvu ya kifedha inayoweza kuziwezesha kufanya vizuri.

Hata hivyo, wadau wa soka nchini wamesema licha ya timu hizo tatu kupewa nafasi kubwa, zipo nyingine zinazoweza kushangaza kutokana na malengo na mipango yao ndani na nje ya uwanja, huku wakieleza matarajio yao ya ligi yenye ushindani mkubwa.

Timu zinazotajwa zaidi kuwa na nafasi ya kumaliza ligi kwa mafanikio na kupanda Ligi Kuu ni Bandari Tanzania, KMC na Mtibwa Sugar, licha ya ukweli kwamba zipo nyingine zinazoweza kubadili matokeo wakati wowote.

Jumla ya timu 16 zinatarajiwa kuchuana kusaka nafasi mbili za kupanda daraja moja kwa moja, huku zitakazomaliza nafasi ya tatu na nne zikicheza mchujo (play-off) kusaka nafasi nyingine ya kupanda Ligi Kuu.


HISTORIA

Kwa misimu takriban sita ni timu tatu pekee zilizowahi kupanda kutoka Championship kupitia mchujo (play-off) baada ya kuzitoa timu zilizokuwa Ligi Kuu Bara. Miongoni mwazo ni Ihefu ambayo kwa sasa inajulikana kama Singida Black Stars ilipoiondoa Mbao FC ya jijini Mwanza.

Ihefu iliyomaliza nafasi ya tatu msimu wa 2020-2021 ilifanikiwa kupanda Ligi Kuu baada ya sare ya jumla ya mabao 4-4 dhidi ya Mbao, ikifaidika na wastani wa mabao mawili ya ugenini, licha ya kufungwa 4-2 katika mchezo wa marudiano uliopigwa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Highland Estate wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Ihefu ikiwa nyumbani iliifunga Mbao FC mabao 2-0, matokeo yaliyowabeba walima mpunga hao kwa jumla.

Mashujaa FC ya mkoani Kigoma nayo ni miongoni mwa timu zilizopanda kupitia ‘play-off’, baada ya kuiondoa Mbeya City kwa jumla ya mabao 3-1. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Mashujaa ilishinda 2-1.

Katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Maafande hao walishinda bao 1-0 na kuishusha Mbeya City iliyokuwa Ligi Kuu, huku wao wakipanda daraja.

Polisi Tanzania ni timu ya tatu kufanya hivyo baada ya msimu uliopita kuikanda Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 4-1 na kufanikiwa kurejea Ligi Kuu kupitia ‘play-off’, hivyo kukamilisha orodha ya timu tatu za Championship zilizoandika historia hiyo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Moshi mkoani Kilimanjaro, Polisi Tanzania iliinyuka Prisons 4-0. Katika mchezo wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Prisons ilishinda 1-0, matokeo ambayo hayakuwa na faida kwao, hivyo kushuka daraja.


CHAMP 01

BANDARI TANZANIA

Licha ya kuwa msimu wao wa kwanza kucheza Ligi ya Championship, Bandari Tanzania inapewa nafasi kubwa ya kupanda Ligi Kuu kutokana na nguvu ya kifedha, usajili wa nyota wenye majina, uwezo na uzoefu wa ligi zenye ushindani.

Timu hiyo inayomilikiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imefanya usajili wa nyota waliowahi kutikisa Ligi Kuu ndani na nje ya nchi, akiwamo Joyce Lomalisa, Sixtus Sabilo, Mohamed Kassim, Ally Ramadhan, William Elias, Issah Ngoah, Ayoub Semtawa na Hajji Ugando.

Uw epo wa wachezaji hao unaweza kuwa kete muhimu kwa timu hiyo katika kufanikisha lengo la kupanda Ligi Kuu.


CHAMP 02

KMC

Timu hiyo iliyowahi kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ni miongoni mwa vigogo watatu wanaopewa nafasi kubwa ya kurejea Ligi Kuu kutokana na ubora wa kikosi, hasa katika usajili walioufanya.

Pia, uzoefu na nguvu ya kifedha ni sehemu ya kete kubwa kwao katika kufanya vizuri, kutokana na kutokuwa na mabadiliko makubwa kikosini ikilinganishwa na msimu uliopita walipokuwa Ligi Kuu.

Maandalizi yake kuanzia nje hadi ndani ya uwanja, yakipewa nguvu na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, ndiyo yanayoifanya timu hiyo kuwa na jeuri ya kuianza na kuimaliza Championship kibabe.


CHAMP 03

MTIBWA SUGAR

Historia yao katika soka la ushindani nchini inawapa matumaini mapya ya kurejea Ligi Kuu baada ya kuwa na matokeo mabaya kwa misimu miwili mfululizo, ikipanda na kushuka daraja.

Uongozi wenye muunganiko, akiwamo Jamal Bayser aliyewahi kuipa mafanikio timu hiyo hadi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu miaka miwili mfululizo, 1999 na 2000, unaweza kurejesha tena rekodi na heshima yao.

Usajili bora walioufanya wa nyota wenye uzoefu na vipaji binafsi, akiwamo Seif Karihe, Issa Abushehe, Shaban Ada, Peter Mwalyanzi, Issa Rashid na Rehan Kibingu kutoka Fanja FC ya nchini Oman, ni turufu kubwa kwa ‘Wakata Miwa’ hao.


CHAMP 04

TMA

Licha ya kutotajwa sana, TMA inaweza kushangaza wengi katika Championship msimu huu kutokana na mabadiliko ya uongozi baada ya kuwa katika mikono mipya ya vigogo.

Timu hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli (Tanzania Military Academy), inadaiwa kuuzwa mkoani Iringa na itacheza mechi zake jijini Mbeya, ikisubiri kukamilika kwa ukarabati wa Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Kutokana na kiu kubwa ya mashabiki na wadau waliyonayo baada ya kukosa uhondo wa Ligi Kuu kwa misimu zaidi ya minne sasa, hali hiyo inaweza kuwa sababu ya vigogo hao kupambana iwezekanavyo kuipandisha timu hiyo.


CHAMP 05

RHINO RANGERS

Siyo jina jipya kwenye medani za soka nchini, kwani kabla ya kushuka daraja ilishafanya makubwa katika Ligi Kuu na sasa inaisaka tena baada ya kupanda Championship msimu huu.

Licha ya kutokuwa na kelele nyingi za kutamba, mipango inayosukwa kimyakimya ndani na nje ya uwanja inaweza kuwasapraizi wengi itakapofanya kweli na kurejesha burudani ya Ligi Kuu mjini Tabora.


CHAMP 06

MBEYA KWANZA

Timu hii ambayo iliasisiwa mkoani Mbeya, kwa sasa imeweka makazi yake mjini Tabora na habari za ndani ni kuwa tayari imeshapigwa bei tangu msimu uliopita, huku vigogo wa mjini Tabora wakihitaji kuona ikirudi Ligi Kuu.

Kwa takribani misimu mitatu mfululizo tangu iliposhuka daraja, imekuwa ikiishia nafasi ya nne na kucheza ‘play-off’ ya kupanda Ligi Kuu, ikiwamo msimu uliopita, lakini imekuwa ikizidiwa kete na wapinzani.

Kutokana na kukosa nafasi ya kurejea Ligi Kuu kwa muda mrefu, huenda msimu huu wa 2026-2027 ikaja kivingine na kukata kiu ya kukosa uhondo huo na kuungana na vigogo wa soka nchini Simba na Yanga.


CHAMP 07

SONGEA UNITED

Timu hiyo ya mjini Songea inashiriki Championship kwa msimu wa tatu mfululizo bila mafanikio tangu ilipokamilisha mchakato wa kuinunua Fountain Gate Talent, lakini sasa imeonekana kuja kivingine.

Tangu Majimaji ishuke daraja, Mkoa wa Ruvuma haujapata tena burudani ya Ligi Kuu na sasa nguvu zimeelekezwa kwa timu hiyo kuona inakata kiu ya mashabiki ambao wamekuwa wakizisikia Yanga na Simba.


CHAMP 08

TANZANIA PRISONS

Pamoja na ukimya wake tangu iliposhuka msimu uliopita, Maafande hao wanaweza kurejea tena Ligi Kuu kutokana na ushawishi wao kwa wadau wa soka, mipango na uzoefu wao katika ligi.

Katika usajili wao wa nyota wengi vijana ambao ni askari, pamoja na mchanganyiko kidogo wa wachezaji raia, wan aweza kuingia kwenye michuano wakicheza kama hawana cha kupoteza na kushangaza mwishoni.

Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini haijawa na matangazo yoyote kuhusu mipango na mikakati yake, ikifanya hesabu zake chini kwa chini na kusubiri kuingia uwanjani kurejesha heshima yao.

Timu nyingine ni Transit Camp yenye uzoefu mkubwa wa ligi, ambayo imekuwa ikiishia nafasi za nne za juu, Bigman FC, Ken Gold, Kigamboni United (zamani B19), Stand United ‘Chama la Wana’, Gunners, Mbuni na IAA SC.

Kufuatia kuanza kwa Championship, mdau wa soka aliyejitambulisha kwa jina la Justine Mwo mbeki, anasema msimu ujao utakuwa wa vita kali kutokana na timu nyingi kul ingana uwezo, japokuwa mipango na mikakati ndiyo inaweza kuzitofautisha, akieleza kuwa ushi ndani utakuwa mkali.

“B andari Tanzania, KMC na Mtibwa Sugar, wawili kati yao watapanda, japokuwa hatuzibezi hizo nyingine kama Prisons, Stand United, Transit Camp, Songea United na TMA,”€  anasema Mwombeki.