Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upotoshaji, propaganda zimejaa sakata la Damaro


WAKATI wa sakata la mkataba wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Bernard Morisson, linaendelea, viongozi wa Yanga hawakuonekana kuyumba. Labda kwa kile walichoonba kuwa walikuwa upande sahihi wa shauri hilo.


Kwamba walijua mchezaji huyo raia wa Ghana alikuwa na mkataba halali na hivyo kusingeweza kuwa na uamuzi wa kubatilisha usajili wake Yanga, na hivyo kutulia kusubiri uamuzi wa mwisho.


Lakini uamuzi uliwapiga butwaa. Shauri ambalo walitegemea litolewe uamuzi wala halikuzingatiwa katika kesi hiyo. Na badala yake wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wakajikita kutafuta kasoro za mkataba ambao shauri lilidai haukuwepo.

Na matokeo yake kamati ikatoka kikaoni ikiwa imegawanyika. Hakukuwa na uamuzi mmoja huku baadhi ya wajumbe wakiwa wamediriki kukiuka maadili kwa kujadili hadharani mambo ya kikaoni hata kabla ya uamuzi kutoka.

Ulikuwa ni uamuzi ulioiacha uchi kamati hiyo muhimu katika kunyoosha mpira wa miguu katika masuala ya sheria na kulinda hadhi za wachezaji. Ilidaiwa kulikuwa na kasoro za mkataba katika eneo moja na hivyo kamati eti kuutangaza mkataba huo kuwa batili, na hivyo kumuweka Morisson huru.

Hali ya sasa ya sakata la usajili na uraia wa kiungo wa Yanga, Mohamed Damaro. Mchezaji huyo alikuwa raia wa Guinea, lakini aliomba uraia wa Tannzania na serikali kumpa utaifa wa Tanzania yeye pamoja na wachezaji wengine watatu.

Wakati huo alikuwa Singida Black Stars kabla ya kusajiliwa na Yanga wakati wa dirisha dogo. Lakini hadhi yake kama Mtanzania sasa inahojiwa na Simba, ambayo inadai taarifa zake katika mfumo wa uhamisho zinaonyesha kuwa bado ni raia wa Guinea, na hivyo inataka mechi alizoshiriki zibatilishwe.

Mazingira yaliyopo sasa ni kama yale ya wakati ule wa sakata la Morisson. Yanga wametulia, wakiamini kuwa hoja zote zinazopingana na uraia wake au uhalali wa usajili wake kama raia wa Tanzania hazina mashiko.

Wachambuzi na wachangiaji mbalimbali wamekuwa wakionyesha kuwa Damaro anacheza soka nchini kinyume cha kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), zinazoeleza taratibu za mchezaji kubalidi uraia na kuwa na sifa za kucheza soka katika taifa lake jipya.

Pia wanasema pamoja na Damaro kusajiliwa kuichezea Singida Black Stars na sasa Yanga, bado taarifa zake kwenye mtandao wa usajili zinaonyesha kuwa bado ni raia wa Guinea, na hivyo anakuwa mcheazaji wa 13 wa kigeni katika orodha ya usajili wa Yanga kinyume na kanuni zinavyotaka wachezaji 12 tu wa kigeni.

Hawa wachambuzi hawajaonyesha sehemu yoyote ambayo kanuni za Fifa zinazungumzia mcheaaji aliyebadili uraia kucheza soka katika ngazi ya klabu kwenye taifa lake jipya.

Wote wananukuu kanuni za Fifa zinazozungumzia kubadili chama au shirikisho la nchi, au kwa Kiingereza ‘ku-swichi’ association. Ni wazi kuwa Fifa haiwezi kuzungumzia masuala ya uraia, kwa kuwa haina mamlaka hayo, bali inazungumzia association au vyama wanachama wake.

Mchezaji anapoomba kuchezea chama kipya cha soka (switch association), maana yake anaomba Fifa imkubalie kuchezea timu mpya ya taifa tofauti na ile ambayo amekulia na pengine ambayo amewahi kuchezea timu zake za taifa za umri. Haimaanishi kuwa anaomba kucheza soka kwenye klabu ya taifa lake jipya.

Hapa ndipo ama kwa makusudi au kwa kutojua wachambuzi na wachangiaji wengi wanapoyumbisha mjadala ama wanalenga kupotosha shauri hili ili ionekane kuna tatizo katika usajili wa Damaro.

Kanuni hizo za Fifa zinaangalia historia ya mchezaji huyo kama ana asili na nchi ambayo anataka kuichezea timu yake ya taifa, na masharti mengine kama kuishi kwa miaka fulani mfululizo kwenye nchi anayotaka kuichezea, na mengine.

Hakuna sehemu inazungumzia masharti hayo kwa mchezaji anayetaka kuchezea klabu ya taifa hilo lake jipya.

Hata huko kupitishwa na vyombo maalum vya soka, wachambuzi wanazungumzia kamati ya sheria na hadhimza wachezaji, ambayo kimsingi kwenye kanuni za Fifa ni ile itakayoridhika na vigezo vyote vya mchezaji kuchezea timu ya taifa ya nchi yake mpya, na si klabu.

Kwa hiyo, unaposikiliza mijadala mingi unaona wazi kuwa kuna watu wanakwepa kuzisoma kikamilifu kanuni hizo ili watoe picha halisi ya shauri la Damaro. Hata hiyo, mtandao wa Fifa kuonyesha Damaro bado ni raia wa Guinea si suala linalohusu mashindano ya ndani ya nchi. Hilo litahusika pale Taifa Stars itakapomhitaji, lakini hilo halitawezekana kwa kuwa umri umeshapita ule wa kuwa na sifa za kuchezea timu ya taifa ya nchi yake mpya.

Kama nilivyozungumzia sakata la Morisson, vyombo vyetu havieleweki. Tumeona Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ilivyofikia uamuzi wa kuipa Morocco ubingwa mezani baada ya Senegal kutwaa ubingwa uwanjani.

Kwa Morisson, shauri halikuwa kasoro za mkataba bali kama amesaini mkataba au la, lakini uamuzi ukawa shauri jipya ambalo halikuwasilishwa mezani mwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Pamoja na kwamba Yanga ina uhakika suala hilo halina utata hata chembe, bado vyombo vyetu vina maamuzi ya mazingaombwe kama yale ya Morisson. Si ajabu hivi sasa inahaha kutafuta kasoro za kuamua tofauti na shauri lilivyo.

Ila, chochote watakachoamua tofauti kinaweza kusababisha msimu ukamalizika tena kwa Rais Samia Suluhu kuingilia kati, kama msimu uliopita ulivyokuwa. Ni muhimu tuheshimu kanuni tulizojiwekea kutuongoza.

Propaganda na nguvu nyingi zisitumike kulazimisha hoja ambayop haipo. Tujikite kwenye mpira na kuachana na siasa za nje ya uwanja.