Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UCHAMBUZI: Mabeki bora wanne wa kati VPL msimu huu

Muktasari:

KATIKA Ligi Kuu Bara msimu huu, baadhi ya mabeki wa kati wameonyesha kiwango kizuri na kusaidia safu za ulinzi za timu zao.

KATIKA Ligi Kuu Bara msimu huu, baadhi ya mabeki wa kati wameonyesha kiwango kizuri na kusaidia safu za ulinzi za timu zao.

Hata hivyo wapo ambao wanaonyesha kitu cha kipekee zaidi kulinganisha na wenzao ambao wanapaswa kupewa sifa za ziada.

Wapo walinzi wa kati wanne ambao bila shaka viwango na uwezo wao msimu huu vinastahili pongezi. Nianze na Joash Onyango wa Simba. Ni msimu wake wa kwanza akiwa ametoka Kenya ambako alikuwa anaichezea Gor Mahia. Ujio wake awali ulishtua kidogo kwa sababu mashabiki wa mpira wana tabia ya kuangalia facial expression (sura za watu)pasipo kuangalia atawapa kitu gani, hivyo walimbeza kwamba aasingeisaidia Simba.

Onyango hakujali kwa sababu ya kujitambua amekuja kufanya kazi alihimili presha ya mashabiki na kuelekeza akili uwanjani.

Amekuja amekuta wachezaji wanaocheza beki wa kati wapo kina Kennedy Juma, Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Ibrahim Ame lakini kwake halikuwa tatizo kwa namna alivyo na akaweza kujihakikishia nafasi dhidi yao.

Sifa ya kwanza ni mchezaji mtulivu na ana uwezo wa kufanya hesabu sahihi pamoja na kwamba hana spidi amekuwa na uwezo wa kuwadhibiti washambuliaji wenye kasi.

Anacheza kwenye nafasi na kufuata maelekezo na anatumia akili. Ni mchezaji ambaye yupo makini na amekuwa msaada kuondosha mipira. Amemsaidia Wawa awe tulivu jinsi anavyomsaidia majukumu na ana uwezo wa kuona hatari na kukabiliana na wapinzani na amekuwa akishirikiana vyema na kipa.

Beki mwingine wa kati ni Iddi Mobi wa Polisi Tanzania. Huyu hatajwi sana lakini ukimuangalia anavyocheza utamjua. Anasoma mchezo, anaweza kutuliza timu, mzuri kwenye matumizi ya nguvu pale inapobidi na anajiamin. Ni mchezaji anaye-offer (anayetoa) vitu vingi. Mwepesi kufanya uamuzi, anaweza kucheza mipira ya vichwa na uwezo wa kutumia maarifa na mbinu nyingi za kiulinzi

Dickson Job ni wa Yanga, naye pia naamini ni miongoni mwa mabeki bora wanne wa kati nchini kwa sasa. Alikuwa mchezaji tegemeo Mtibwa Sugar.

Ni mchezaji upcoming (anayechipukia) anayeonyesha atakuwa beki bora wa kati kutokana na timing, ball control (udhibiti wa mpira), anaanzisha mashambulizi na mzuri wa kubadili uelekeo wa mpira na ni mara chache ananyanyua mipira au power play (mzuri katika michezo ya nguvu).

Mechi zote ambazo amecheza kumekuwa na clean sheet (hawakapoteza) na ameonyesha kuzoea haraka Yanga. Hiyo inamfanya aendelee kuaminiwa na kupewa nafasi. Kiwango chake anacheza mpira wa kisasa, anabadilika kulingana na aina ya timu. Ana final rythm (umaliziaji mzuri). Ni detective player (anabaini dosari haraka) na anaisaidia Yanga kwa kuingia kwenye mfumo, lakini ni mzuri katika combined defensive sytem (ulinzi shirikishi). Ana discipline (heshima) ya kutosha nje na ndani ya uwanja. Ni mchezaji ambaye ana dhamira ya kucheza soka na ana easy going personality (mwepesi wa kusonga mbele).

Mchezaji wa mwisho ambaye anastahili kutazamwa kama mmoja wa walinzi wanne wa kati bora nchini kwa sasa ni Luseke Kigi wa Mtibwa. Timu yake huenda ikashuka daraja lakini yeye akawa lulu timu nyingine. Ana tabia zinazofanana na Job. Marking (umakini), timing (umahiri) na determination (uamuzi) yake ni vya hali ya juu na ana high concentration pamoja na physical quality (ubora wa thamani).