Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba inavyofukuzia rekodi ya kushangaza ya Yanga

PUMZI Pict


SARE ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance ya Tunisia katika Uwanja wa Mkapa imeipatia Simba alama ya kwanza kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.


Hata hivyo, Simba iko kwenye hali mbaya ikiburuza mkia kwa kugeuka kuwa kibonde katika kundi lake. Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Mnyama kufanya hivyo tangu ianze kushiriki kwa mara ya kwanza 2003 mashindano hayo.


Mara zote ambazo Simba ilishiriki hatua hii ama ilivuka kwenda robo fainali au ilizidiwa alama chache na aliyevuka, lakini sio kuwa wa mwisho katika kundi.

PUMZ 01

HATUA YA MAKUNDI

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), lilianzisha hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika 1997.

Simba imeshiriki hatua hiyo mara kibao ikiwa ni 2003, 2018/19, 2020/21, 2021/22, 2022/23, 2023/24, 2024/25 na msimu huu wa 2025/26. Hata hivyo, timu ya kwanza hapa nchini kufuzu hatua hiyo ilikuwa Yanga, 1998.

Lakini, Yanga ni kama walikwenda kujifunza kwani walimaliza na sare mbili tu, wakifungwa mechi nne kati ya sita.

Matokeo ya Yanga yalikuwa; 1-1 Manning Rangers, Asec Mimosas 2-1 Yanga, Raja 6-0 Yanga, Raja 3-3 Yanga, Manning Rangers 4-0 Yanga na Yanga 0-3 Asec Mimosas.


KUNDI B 1998

1. ASEC Mimosas    6        4        1         1         10      4        13

2. Ikapa Sporting   6        3        1         2        9        6        10

3. Raja                   6        2        2        2        12       7        8

4. Yanga                6        0       2        4        5        19       2

PUMZ 02

Hayo yanabaki kuwa matokeo mabaya zaidi kwa Yanga, lakini, walifuzu tena hatua ya makundi na safari hii Kombe la Shirikisho 2016. Huko wakaangukia Kundi A pamoja na TP Mazembe, Mo Bajaia ya Morocco na Medeama ya Ghana.

Japo safari hii Yanga walijitahidi kidogo angalau wakapata alama nne, lakini waliendelea kuburuza mkia.

Matokeo ya Yanga katika kundi A la mashindano hayo yalikuwa;  Mo Bajaia 1-0 Yanga, Yanga 0-1 TP Mazembe, 

Yanga 1-1 Medeama, Medeama 3-1 Yanga na Yanga 1-0 Mo Bajaia


KUNDI A 2016

1. TP Mazembe       6        4        1         1         10      13

2. MO Bejaia          6        2        2        2        2        8

3. Medeama          6        2        2        2        8        8

4. Yanga                6        1         1         4        4        4

PUMZ 03

Baada ya hapo walirudi tena 2018 na kuangukia kundi D pamoja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda pamoja na Gor Mahia ya Kenya. Yanga walipata tena alama nne, lakini wakabaki wa mwisho kwenye kundi.

Matokeo yalikuwa USMA 4-0 Yanga, Yanga 0-0 Rayon Sports, Gor Mahia 4-0 Yanga, Yanga 2-3 Gor Mahia, Yanga 2-1 USMA na Rayon Sports 1-0 Yanga


KUNDI D 2018

1. USM Alger            6      3        2        1         10      5        11

2. Rayon Sports     6       2        3        1         6        5        9

3. Gor Mahia           6       2        2        2        10      7        8

4. Yanga                 6       1         1         4        4        13       4

PUMZ 04

Baada ya hapo wakapotea hadi 2022/23 waliporudi kwa kishindo na kufika fainali ya Kombe la Shirikishp. Hapo sasa wakawa wameliepuka jinamizi la kuwa wa mwisho kwenye kundi, kwani misimu iliyofuata; 2024/25, 2024/25, na sasa 2025/26 walikwepa kuwa wa mwisho. Sasa kitambaa hicho hicho kimeangukia kwa watani zao, Simba.

Ili kuepuka kuwa wa mwisho, Simba watapaswa kupiga hesabu za TUKIWAKI yaani TUKIshinda, WAKIfungwa.

Kwanza ushinde mechi zako na kuwaombea wenzako waharibikiwe kwenye mechi zao. Kwa kawaida hesabu hizo hupigwa na timu inayopigania kufuzu kwenda hatua inayofuata, lakini Simba wanapiga hesabu za TUKIWAKI ili kukwepa kuwa wa mwisho kwenye kundi.

PUMZ 05

Hii itakuwa aibu kubwa kwa Simba, sawa na kushuka daraja. Simba ndio imekuwa mkombozi wa soka la Tanzania kimataifa. Mashindano ya Afrika kwa klabu yalianza 1965; Klabu Bingwa Afrika.

Timu ya kwanza nchini kushiriki ilikuwa Cosmopolitan, mabingwa wa 1967. Walitakiwa kushiriki 1968, lakini walishindwa kusafiri kwenda Somalia. Wakaja Yanga wakashiriki kuanzia 1969 hadi 1973. Simba wakashiriki mara ya kwanza 1974 na kufika nusu fainali moja kwa moja.

1993 wakacheza fainali ya CAF, na 1994 robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika. Na hata zilipoletwa hizi hatua za makundi, bado Simba hawakuwahi kuburuza mkia.

PUMZ 06

LIGI YA MABINGWA (2003)

Ikifanikiwa kuwatoa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa, Zamalek ya Misri, Simba iliangukia kundi A. Simba ilimaliza na alama saba nyuma ya Ismailia ya Misri na Enyimba ambayo ilikwenda kuwa bingwa.


KUNDI A

1. Enyimba             6        4        0       2        14       11        12

2. Ismailia             6        3        2        1         13       7        11

3. Simba                6        2        1         3        7        10      7

4. Asec Mimosas    6        1         1         4        6        12       4

PUMZ 07

2018/19

Baada ya kupotea kwa miaka mingi, Simba ilirudi tena kwa kishindo msimu wa 2018/19 na kuangukia kundi D sambamba na Al Ahly ya Misri, AS Vita ya DR Congo na Smouha ya Algeria. Ikamaliza katika nafasi ya pili ikiwa na  alama tisa na kufuzu robo fainali.


LIGI YA MABINGWA (2020/21) 

Simba iliangukia kundi A pamoja na AS Vita ya DR Congo, Al Ahly ya Misri na El Merreikh ya Sudan. Sio tu ilifuzu robo fainali, bali iliongoza kundi mbele ya Al Ahly.


KOMBE LA SHIRIKISHO (2021/22) 

Walianzia Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa katika raundi ya pili wakati huo sheria ziliruhusu kuangukia Kombe la Shirikisho kwa timu zilitolewa katika raundi hiyo.

Simba ilifaidika na sheria hiyo na kujikuta kwenye kundi D pamoja na RS Berkane ya Morocco, Asec Mimosas ya Ivory Coast na US Gendermarie ya Niger. Ikamaliza katika nafasi ya pili na kufuzu robo fainali.

PUMZ 08

LIGI YA MABINGWA (2022/23)

Msimu huo ilifuzu hatua ya makundi na kupangwa kundi C sambamba na Raja Casablanca ya Morocco, Horoya ya Guinea na Vipers ya Uganda. Ilipoteza mechi mbili za kwanza, lakini ilirudi kwa kishindo na kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi, ikafuzu robo fainali.


LIGI YA MABINGWA (2023/24)

Simba ilifuzu tena robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi B lililokuwa na Wydad, Asec Mimosas na Jwaneng Galaxy. Alama tisa ilizovuna zilitosha kuiweka katika nafasi ya pili kwenye kundi, na kufuzu robo fainali.


SHIRIKISHO (2024/25)

Simba ilifunga kazi kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho msimu huo. Ikitokea kundi A lililokuwa na CS Constantine ya Algeria, klabu kongwe kuliko zote Afrika, Bravos ya Angola na CS Sfaxien ya Tunisia iliongoza kundi kwa kishindo.

Kundi hilo ndilo lililozaa msemo wa KUGAWA UTAMU uliobuniwa na Ahmed Ally akiwalenga CS Sfaxien kama vibonde wa kundi. Sasa msemo huo umewarudia wenyewe na kuiga tabia za Yanga za kuburuza mkia kwenye kundi walizokuwa nazo miaka ya nyuma.