Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salman Khan anazidi kuzikusanya tu

ATM Pict

Muktasari:

  • Mbali ya maudhui ya filamu hiyo, stori pia ilikuwa ni faida ambayo ilipatikana. Sikandar ilitengenezwa kwa gharama ya Dola 25 milioni tu lakini iliingiza faida ya takribani Dola 180 milioni hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi huu.

MUMBAI, INDIA:MWANZONI mwa mwaka huu, jina la nyota mkubwa wa Bollywood, Salman Khan, lilirudi tena kwenye vichwa vya habari baada ya kuachia filamu mpya ya Sikandar chini ya kampuni yake ya Salman Khan Films (SKF).

Mbali ya maudhui ya filamu hiyo, stori pia ilikuwa ni faida ambayo ilipatikana. Sikandar ilitengenezwa kwa gharama ya Dola 25 milioni tu lakini iliingiza faida ya takribani Dola 180 milioni hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi huu.

Kiasi hicho cha pesa kimemfanya kuendelea kuwa mmoja kati ya wasanii matajiri na sasa anakaribia kufikia utajiri wa Dola 400 milioni. Hapa tumekusogezea mchanganuo kamili wa utajiri wake na jinsi anavyopiga pesa.

AT 05

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa, utajiri wa Salman Khan unakadiriwa kufikia Dola 380 milioni ambao umetokana na mali na pesa anazoingiza kupitia madili mbalimbali.

Kupitia  filamu moja jamaa anadaiwa kuingiza zaidi ya Dola 30 milioni na kuna baadhi ya muvi zinampa takribani Dola 50 milioni.

Mbali ya filamu, pia ana biashara zake mwenyewe kama kampuni yake ya uzalishaji filamu ya (SKF) ambayo kwa mwaka humpa zaidi ya Dola 10 milioni.

Vilevile anamiliki hisa katika kampuni mbalimbali. Kwa sasa pia anapata mapato kutoka katika kipindi chake maarufu cha televisheni cha Bigg Boss India.

Mwaka 2024 pekee, alitajwa na jarida la Forbes India kama mmoja wa wasanii 10 wanaolipwa zaidi nchini humo, akiwa na mapato ya zaidi ya Dola 50 milioni kwa mwaka.

Vilevile anafanya kazi ya ubalozi na kampuni mbalimbali kama Pepsi, Suzuki, Being Human Clothing (brand yake binafsi), Realme, Emami na Mountain Dew, ambazo zinakadiriwa kumpa jumla ya Dola 25 milioni kwa mwaka.

AT 03

MIJENGO

Anaishi katika jengo la kifahari lililopo eneo la Bandra, Mumbai, ambako ana nyumba yenye thamani ya takribani Dola 8 milioni.

Aidha, anamiliki nyumba nyingine za kifahari maeneo kama Panvel Farmhouse, nje kidogo ya Mumbai, yenye thamani ya Dola 15 milioni ambayo ndani yake ina bwawa, uwanja wa kucheza mchezo wa kukimbia na farasi, chumba cha mazoezi na bustani kubwa.

Vilevile ana nyumba maeneo ya Gorai Beach, yenye thamani ya Dola 5 milioni  aliyoijenga maalum kwa ajili ya mapumziko ya familia.

AT 04

NDINGA

Range Rover Autobiography -Dola 250,000

Mercedes-Benz GLS 600 Maybach -Dola 300,000

Toyota Land Cruiser -Dola 150,000

Audi RS7 – Dola 140,000

Porsche Cayenne Turbo - Dola 180,000

Suzuki Hayabusa - Dola 20,000

Yamaha R1 - Dola 18,000

Kwa ujumla staa huyu anamiliki magari na pikipiki zaidi ya 25.

AT 01

MSAADA KWA JAMII

Khan husaidia sana jamii kupitia taasisi yake ya Being Human Foundation.

Kupitia taasisi hiyo, amekuwa akifadhili elimu, huduma za afya na kusaidia watoto wenye ulemavu.

Mwaka 2023, taasisi hiyo iliripoti kutumia zaidi ya Dola 10 milioni katika miradi mbalimbali ya kijamii huko India.

Pia, aliwahi kutoa misaada maalum kwa waathirika wa mafuriko ya Kerala na wakati wa janga la virusi vya Corona.

AT 02

FAMILIA NA BATA

Salman ni mtoto wa mwandishi maarufu wa filamu Salim Khan. Hadi sasa hajaoa lakini amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mastaa kadhaa wa Bollywood akiwamo Aishwarya Rai, Katrina Kaif, na Iulia Vantur.

Amezungumzia mara kadhaa katika mahojiano kwamba ndoa kwake ni jambo la binafsi na hajahisi muda sahihi au mtu sahihi amefika.

Anapenda kutumia muda wake wa mapumziko akiwa na familia yake, hasa ndugu zake Arbaaz, Sohail na Alvira.