Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya kumsaka malkia mpya wa soka Bara inaanzia hapa

WANAWAKE Pict

Muktasari:

  • Kupigwa kwa mechi hizo ina maana kwamba ufunguzi wa rasmi wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara utakuwa umefanyika na hivyo, kwa mashabiki wataanza kujionea ubora wa mastaa waliosajiliwa na timu 12 zitakazoumana kusaka ubingwa ambao watetezi wake ni JKT Queens.

HATIMAYE ile siku ndo leo. Ule mtanange wa nusu fainali mbili za Ngao ya Jamii kwa wanawake utapigwa kwenye Uwanja wa KMC Mwenge, Dar es Salaam kwa kukutanisha timu zilizomaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu (W) msimu uliopita.

Kupigwa kwa mechi hizo ina maana kwamba ufunguzi wa rasmi wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara utakuwa umefanyika na hivyo, kwa mashabiki wataanza kujionea ubora wa mastaa waliosajiliwa na timu 12 zitakazoumana kusaka ubingwa ambao watetezi wake ni JKT Queens.

Nusu fainali ya kwanza itakuwa kati ya Simba Queens ikiwakaribisha wazee wa Mapigo na Mwendo, Mashujaa Queens saa 7 mchana na ile ya pili itakuwa kati ya mabingwa watetezi JKT Queens dhidi ya Yanga Princess.

Fainali inatarajiwa kupigwa Oktoba 12 uwanjani hapo na tangu michuano hiyo ianzishwe mwaka 2023, JKT imecheza fainali zote mbili.

Fainali ya kwanza ilipoteza mbele ya Wekundu wa Msimbazi Simba kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.

Ile ya mwaka jana timu hiyo ilichukua taji hilo baada ya kuitandika Yanga Princess bao 1-0 likifungwa na Donisia Minja aliyepiga frii-kiki ya kutokea nje kidogo ya kumi na nane.

Leo timu hizo zilizomaliza ndani ya Top 4 kwenye msimamo zinakutana tena wakati ambao JKT ilimaliza kileleni mwa msimamo wa ligi kwa pointi 47 sawa na Simba Queens iliyomaliza nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga.

Kwenye mechi 18 JKT ilifunga mabao 70 na kuruhusu saba huku Simba ikifunga mabao 57 na kuruhusu 15, Yanga ilimaliza nafasi ya tatu kwa pointi 39 ikifunga mabao 39 na kuruhusu 15 wakati Mashujaa iliyomaliza katika nafasi ya nne kwa pointi 31 iliweka nyavuni mabao 33 na kuruhusu 21.

WANA 03

JKT QUEENS vs YANGA PRINCESS

Hii ni mara ya pili timu hizo zinakutana tangu michuano hiyo kuanzishwa mwaka 2023 ambapo Simba Queens iliibuka mabingwa wa kwanza.

Wamekutana mara 18 kwenye mashindano mbalimbali yale ya Ligi Kuu na Ngao ya Jamii tangu mwaka 2018, na Yanga imeshinda mara moja tu ikikumbana vichapo mara 17.

Lakini kwenye mashindano hayo hii inakuwa mara ya pili kukutana, mara ya mwisho ilikuwa fainali ya mwaka jana na JKT ikanyakua taji hilo baada ya kuwatandika wananchi hao bao 1-0 katika fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC.

Leo timu hizo zinakutana tena wakati ambao kila moja imefanya maboresho kwenye maeneo mbalimbali ambayo waliamini msimu uliopita yalikuwa na upungufu.

Kwenye usajili msimu huu timu hiyo iliachana na kocha Ester Chabruma aliyeipa ubingwa timu hiyo wa Ligi Kuu, Ngao ya Jamii na CECAFA kisha ikamsajili Abdallah Kessy ambaye tayari ameipeleka timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayotarajiwa kuanza kuchezwa Novemba nchini Algeria.

Pia imeongeza wachezaji 10 katika dirisha kubwa la usajili na asilimia kubwa ya wachezaji ni vijana waliowatoa kwenye akademi mbalimbali nchini.

WANA 02

Wachezaji hao ni Ester Maseke, Winfrida Castor, Asha Mrisho, Asha Rashid ‘Mwalala’, Winfrida Mungwa, Fumukazi Ally, Mwajabu Mziray, Salma Mohamed, Angel Joseph na Aneth Idama.

Kati ya hao 10 watatu pekee ndio wameingia kwenye kikosi moja kwa moja, Maseke (Bunda Queens) ambaye amekuwa na mwanzo mzuri akicheza kwenye mashindano ya CECAFA na kuipa ubingwa timu hiyo, Mwalala (Simba Queens) ambaye ni mzoefu kwenye ligi hiyo pamoja na Fumukazi aliyetokea Mashujaa Queens.

Hivyo msimu huu tangu timu hiyo ilipocheza mashindano ya CECAFA hakuna mabadiliko makubwa kwa wale waliosajiliwa.

Kwa upande wa Yanga Princess wameendelea na kocha Edna Lema aliyekuwepo msimu uliopita na imeongeza nyota saba watatu wazawa Yasinta Kaluwa (Mbeya), Maimuna Hamis ‘Mynaco’(Zed FC, Misri) na Ester Kolonely (Mlandizi Queens). Wengine ni Wincate Kaari (Kenya) ,Ritticia Nabbosa (Uganda), Precius Christopher na  Ogbonna Akudo (Nigeria).

Hata hivyo wameongeza baadhi ya nyota ambao wanakwenda kuongeza ushindani kwenye kikosi ambacho msimu uliopita kilifanya vizuri na kuleta ushindani WPL.

Kwa takwimu za wachezaji waliosajiliwa huu na wale waliokuwapo awali ni wazi timu hizo zinakwenda kuonyesha upinzani kwenye michuano hiyo.

Uimara wa Yanga upo kwenye eneo la ulinzi na kiungo kuanzia kwa golikipa Rita Akarekor na mabeki wa kati Angela Chineneri na Igwe Uzoamaka ambao wamekuwa na pacha nzuri tangu msimu uliopita wakicheza kwa kuelewana huku eneo la kiungo kuanzia mkabaji Agnes Pallangyo akisaidiana na Aregash Kalsa na Adebis Ameerat.

Inakuwa mechi ngumu kutokana na aina pia ya kikosi cha JKT ambacho uimara wake upo karibu kila eneo kuanzia kwa kipa Naijat Abbas ambaye msimu uliopita aliruhusu lango lake kutikiswa mara saba akiongoza kwa cleansheet.

Eneo jingine tishio kwa timu hiyo ni kwa upande wa washambuliaji likiongozwa na Stumai Abdallah aliyemaliza kinara wa ufungaji na mabao 28, Jamila Rajabu ambaye pia ni mfungaji bora wa mashindano ya CECAFA msimu huu akiweka kambani mabao matano na Mwalala.

WANA 04

SIMBA QUEENS vs MASHUJAA QUEENS

Hii ni mara ya tatu timu hizo zinakutana lakini ikiwa ni ya kwanza kwenye mashindano hayo ambayo Simba imecheza mara mbili na kuchukua ubingwa mara moja.

Kwenye ligi timu hizo zilikutana mara mbili zikitoka sare moja 2-2 Mei 12 mwaka huu na ile 2-0 ambapo Mashujaa ilipoteza dhidi ya mabingwa mara nne wa WPL, Simba Queens.

Timu zote zinakutana msimu huu zikiwa zimefanya maboresho kuanzia neo la benchi la ufundi na kuongeza wachezaji.

Mashujaa Queens ambayo ni msimu wake wa pili kuchezea WPL, imesajili Zuhura Mlekwa (Mwanga City), Sharifa Hamidy (Fountain Gate Princess), Gelwa Yona (Simba Queens), Bhoke Mganda (Bunda Queens).

WANA 01

Kwa Simba imeomungeza, Zainah Nadende (Uganda), Elizabeth Nashoni (Tanzania), Elizabeth Mkuki (Tanzania), Ruth Aturo (Uganda), Zawadi Usanase (Rwanda), Cynthia Musungu (Kenya)

Fasila Adhiambo (Kenya), Neema Mtunzi (Tanzania), Asha Omary (Tanzania), Magnifique Umutesiwase (Rwanda) na Odoma Amarachi (Nigeria).

Asilimia kubwa ya wachezaji waliosajiliwa Simba wametoka ligi mbalimbali na zenye ushindani tofauti na Mashujaa ambao wameongeza nyota waliokuwa kwenye akademi kama Fountain.

Hata hivyo mbali na usajili huo kuna vita ya makocha wazawa kwenye timu hizo, Mashujaa imeendelea na Ally Ally miongoni mwa makocha walioipa mafanikio makubwa JKT wakati anafundisha kabla ya kutimuliwa mwaka 2023 na nafasi yake ilichukuliwa na Chabruma ambaye pia aliondoka.