Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PUMZI YA MOTO: Jux, Vanessa Mdee 'wanapouzika' mgogoro wa Tanzania, Nigeria

JUX Pict

Muktasari:

  • Biafra ni jimbo lililojitenga kutoka Nigeria, mwaka 1967 wakati wa vita vya kiraia nchini humo na kujitangazia uhuru.

MOJA ya makosa ambayo mwalimu Julius Nyerere amewahi kukiri kuyafanya wakati wa utawala wake na kuyajutia ni kuitambua Jamhuri ya Biafra.

Biafra ni jimbo lililojitenga kutoka Nigeria, mwaka 1967 wakati wa vita vya kiraia nchini humo na kujitangazia uhuru.

Serikali ya Tanzania chini ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere ilitangaza kuitambua Biafra kama nchi kamili.

Hii ndiyo sababu ya pale Kinondoni B kuwa na sehemu inayoitwa Biafra...ilipewa jina hilo kwa heshima ya jimbo lile la Nigeria lililojitenga.

Nigeria haikuwahi kumuelewa Nyerere kuunga mkono watu wanaojitenga wakati yeye ni mmoja wa viongozi shupavu wa Afrika wanaohubiri muungano wa bara hili.

Hata Mwalimu mwenyewe baada ya kustaafu aliwahi kujutia uamuzi ule akisema hakupaswa kuiunga mkono Biafra kujitenga kwa sababu kama mwanamajumui wa Afrika, aliamini katika umoja na sio utengano.

JU 01

Mwaka 1970 Nigeria ikairudisha kundini Biafra na baadaye kidogo kidogo hasira za Nigeria kwa Nyerere na Tanzania kwa jumla zikaisha.

Hata mwaka 1977 Nyerere alipofanya ziara ya kiserikali nchini humo, alipokewa kwa heshima zote na Rais Olusegun Obasanjo wa nchi hiyo.

Peleka mbele hadi mwaka 2005, miaka zaidi ya 50 baadaye, Tanzania na Nigeria zinagonga tena vichwa vya habari, lakini safari hii siyo kwa tofauti za kidiplomasia bali kijamii.

Vijana wanne kutoka mataifa haya mawili wanafukia katika kaburi la sahau tofauti zile na kutengeneza muunganiko mpya wa damu, roho na mwili.

Vijana hao ni Juma Jux na Vanessa Mdee kutoka Tanzania, na Rotimi na Priscilla Ojo kutoka Nigeria.

Juma Jux na Vanessa Mdee ni majina makubwa Tanzania, wakifahamika zaidi kupitia sanaa ya muziki.

Rotimi na Priscilla Ojo pia ni majina makubwa Nigeria, wakifahamika kwa namna tofauti.

Rotimi ni msanii mkubwa anayefanyia kazi zake nchini Marekani, akiigiza na kufanya muziki.

JU 02

Priscilla Ojo ni maarufu zaidi kupitia jina la baba yake, Iyabo Ojo, ambaye ni muigizaji mkubwa sana Nigeria. Hata hivyo, Priscilla mwenyewe pia ni muigizaji.

Picha ilianza mwaka 2019 kwa Rotimi kutoka Nigeria kuweka wazi mahusiano yake na Vanessa Mdee wa Tanzania.

Mwaka mmoja nyuma, 2018, Vanessa alitoka kuachana na Juma Jux aliyedumu naye kwa miaka sita kwenye mahusiano.

Wakati huo Rotimi alikuwa aking'aa kama Andre 'Dre' Coleman kwenye tamthilia ya Power iliyotengenezwa na kina 50 Cent...Rotimi alikuwa wamoto sana!

Mahusiano yao yamewapatia watoto wawili na bado wanatamba nayo.

Hakuna Mtanzania mnyonge, Jux naye akazama Nigeria na kuibuka na 'mtoto' Priscilla na sasa wamefunga ndoa.

JU 03

Na zaidi ya hapo, Priscilla amebadili kabisa dini ili kuifuata dini ya mumewe ambaye ni muislamu.

Kwa hiyo siyo tu Jux na Priscilla wameunganisha nchi mbili, bali pia wameunganisha dini, ambayo ni moja ya sababu kuu za Biafra kutaka kujitenga wakati ule.

Mikasa ya mapenzi ni moja ya simulizi zenye kuvutia kwa upande mmoja na kuhuzunisha kwa upande mwingine.

Moja ya simulizi hizo ni ile ya wanasiasa wawili mashuhuri wa Uganda; Rais Yoweri Museveni na mpinzani wake mkuu, Kizza Besigye.

Mke wa Kizza Besigye, Winnie Byanyima, alikuwa mpenzi wa Yoweri Museveni wakati wa vita vya msituni kuisaka serikali.

Wakati huo Besigye alikuwa daktari wa Museveni na Winnie akiwa mpiganaji aliyeamua kuuweka urembo pembeni na kuvaa kombati.

Binti huyo msomi wa chuo kikuu cha Manchester Uingereza katika fani ya uhandisi, aliamua kuingia msituni baada tu ya kurudi kutoka masomoni Uingereza kama hasira zake kwa serikali kufuatia kushuhudia binamu yake aliyeitwa James Kanyamunyu kuuawa na serikali ya Idd Amin wakati wakisoma chuo kikuu cha Makerere.

JU 04
JU 04

Ndipo akatoroka na kwenda Uingereza kusoma...aliporudi  akaingia msituni kuungana na Museveni.

Huko akatumbukia penzini na Museveni ambaye tayari alikuwa amemuoa Janet tangu mwaka 1973.

Baada ya kushinda vita mwaka 1986 na Museveni kuchukua serikali, akapeleka posa kwa wazazi wa yule binti ili aoe kabisa...lakini baba wa binti akakataa kuipokea na penzi likavunjikia hapo.

Baba alikataa kwa sababu hakuwahi kumkubali Museveni kwani alimfahamu tangu akiwa kijana mdogo. Mzee huyo alikuwa mwalimu katika shule ambayo Museveni alisoma, Mbarara High School, miaka ya 1950.

Hakuwa tu mwalimu wake bali alimlea kama mwanaye na kuna wakati alikaa naye nyumbani kwake...kwa hiyo anamjua vizuri sana.

Baada ya penzi la Museveni na Winnie kuvunjika, binti akaangukia kwa Kizza Besigye, yule daktari wa Museveni kule msituni walikokuwa wote.

Wakati huo Besigye naye alikuwa ameshakorofishana na Museveni na kuwa mkosoaji wake mkuu na baadaye mpinzani wake mkuu.

Penzi la Winnie likakoleza uhasama wao uliohamia katika kuwania penzi la nchi yao kupitia kura za wananchi.

Kuanzania uchaguzi mkuu wa 2001 hadi sasa Besigye na Museveni wanawindana kama chui na paka.

Yote ni sababu ya mapenzi!