Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pedro anavyorudisha makali Yanga

YANGA Pict


YANGA imeanza kutulia na jana Jumapili Novemba 9, 2025 ikapata ushindi mkubwa zaidi tangu kuanza kwa msimu huu ikiichapa KMC mabao 4-1.


Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, walipata ushindi huo kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar ikiwa ndiyo klabu ya kwanza msimu huu kushinda kwa idadi kubwa zaidi kwani awali ushindi mkubwa uliokuwa umewekwa tangu ligi kuanza ulikuwa mabao 3-0, Simba ikiwa vinara ikifanya hivyo mara mbili.


Matokeo ya jana ikiwa ni mechi ya pili kwa kocha mpya wa watetezi, Pedro Goncalves yameifanya Yanga kukaa kileleni mwa msimamo ikifikisha pointi 10 baada ya kushuka uwanjani mara nne, ikishinda tatu na kutoka sare moja na kufunga mabao tisa na kuruhusu moja.

Yanga ya Pedro ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya jana kupambana kwa nguvu kubwa hasa kipindi cha pili na kupata matokeo hayo yaliyoibeba timu hiyo kongwe.

Ushindi huo umezidi kuididimiza KMC mkiani mwa msimamo ikicheza mechi sita na kuvuna pointi tatu tu, ikishinda mechi moja na kupoteza tano, huku ikifunga mabao mawili na kufungwa 10, ikiwa ndiyo timu yenye safu dhaifu ya ushambuliaji na ukuta mwepesi hadi sasa Bara.

YANG 01

VITU VYA PEDRO

Mashabiki wa Yanga jana walitaka kuangalia kocha wao mpya Pedro atakuja na kipi kipya baada ya kukaa na timu hiyo kambini takribani wiki moja na zaidi akianza kukitengeneza kikosi chao.

Yanga jana, ilianza kuonnyesha inatulia, inapiga pasi za kwenda mbele na mipango ikianza kurudi katika kujenga mashambulizi yao kama ilivyokuwa kabla ya msimu uliopita kumalizika.

YANG 02

WANAKABA

Mabadiliko mengine ni namna wachezaji wa Yanga walivyoanza kurudisha nidhamu ya ukabaji na kwa namna kikosi hicho kilivyocheza jana, ilikuwa kila mchezaji mara baada ya mpira kutoka kwenye umiliki wake anatakiwa haraka kuutafuta.

YANG 07

PUMZI INAREJEA

Kabla ya ujio wa Pedro kulikuwa na kelele kikosi cha Yanga kinakata pumzi, hii ilitokana na kipindi cha pili karibu na mwishoni kilikuwa kinateseka kikiutafuta sana mpira.

Hata hivyo, kama ambavyo Mwanaspoti lilikujulisha wiki iliyopita, kulikuwa na kazi kubwa ya kupandisha pumzi na stamina hatua ambayo jana ilionekana na mambo kubadilika.

Yanga hadi mwisho wa mchezo, ilionekana bado inaweza kushambulia na kutamani ushindi, ni vile tu muda wa mchezo ulikuwa umetimia kwa mujibu wa mwamuzi Hassan Katanga kutoka Tabora.

YANG 03

PACOME NI YULEYULE

Staa wa mchezo huo alikuwa kiungo Pacome Zouzoua, jamaa bado yupo kwenye daraja lilelile la ubora, Yanga inatembea kwenye mabega yake, akiamua muda gani ifunge au kufanya balaa kwenye lango la wapinzani.

Pasi zake za haraka akikutana na wenzake wanaozijulia kama Maxi Nzengeli inakuwa hatari zaidi kwa wapinzani, kiwango chake hakihitaji muda mrefu akiwa uwanjani kugundua jamaa ni staa muhimu wa Yanga.

YANG 04

BOYELI KAANZA, DUBE BADO

Mshambuliaji Andy Boyeli jana aliingia akitokea benchi na kufunga mabao mawili yakiwa ni mabao yake ya kwanza kwenye ligi lakini baada ya mchezo mashabiki wa timu hiyo wakampongeza kwa kumpa fedha kama kawaida yao.

YANG 08

Wakati Boyeli anaanza kazi, mwenzake Prince Dube ambaye alianza mchezo huo bado yuko kwenye kipindi kigumu cha ukame wa mabao akihitaji utululivu zaidi ili kurudisha ufalme wake.

YANG 06

BEKI UTULIVU MDOGO

Ukuta wa Yanga bado haujatulia sawasawa licha ya KMC kupata bao moja, lakini kulikuwa na uwezekano wa kufunga zaidi kama wangetulia kutokana na mabeki wa kati Bakari Mwamnyeto na msaidizi wake Dickson Job ni kama wanakata mawasiliano.

Hili linatakiwa kuimarishwa zaidi kabla ya kwenda kucheza mechi ngumu na kubwa za hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Affrika wiki chache zijazo.

YANG 05

KMC INA KIBARUA

Licha ya KMC kuwa chini ya kocha mwenye cv kubwa, Marcio Maximo na kucheza vyema kipindi cha kwanza cha mechi ya jana, lakini bado ina kibarua cha kuhjinasua mkiani kutokana na timu kukosa muungano mzuri na kutengeneza nafasi za kutosha.

Wachezaji wa eneo la mbele la KMC kuanzi viungo hadi washambuliaji wanacheza kwa uwoga sana na hata jana kama wangekuwa na utulivu na kujipanga vyema isingekuwa ajabu kutoka na ushindi mbele ya Yanga, hasa kipindi cha kwanza kwani watetezi walikuwa hovyo ila utulivu mdogo wa nyota hao wa Wana Kino ukawaangusha na kuambulia bao moja tu.

Bao lenyewe likiwa ni kosa lililofanywa na kipa Diarra Djigui aliyeupangua vibaya mpira wa shati Rashid Chambo na kumfanya Daruwesh Saliboko lililokuwa bao la pili kwake msimu huu, likiwa pia ni la pili kwa timu hiyo kuonyesha namna gani ilivyo dhaifu katika eneo hilo kwa msimu huu.

KMC ni mechi moja pekee ambayo ilicheza bila kuruhusu wavu wake kuguswa na ni ile ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Dodoma Jiji, lakini mechi nyingine zote tano zilizofuta imeruhusu wastani wa mabao mawili, kwani ilianza kwa kufungwa na Singida BS 1-0, Tanzania Prisons (1-0), Mbeya City (3-0), Fountain Gate (1-0) na Yanga 4-1).