Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota hawa tumaini jipya la Afrika 2026

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Baada ya mafanikio hayo Afrika imepata nafasi ya kupeleka wawakilishi 10 kwa mara ya kwanza baada ya FIFA kuongeza idadi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kutoka timu 32 hadi 48.

MIAMI, MAREKANI: NDOTO ya Afrika ni kuona mmoja kati ya mataifa 10 wakiweka rekodi kufika fainali kama si kutwaa ubingwa kwa Kombe la Dunia itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, 2026.

Ndoto ya kutwaa kombe hilo imepewa nguvu hasa baada ya

Morocco kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika nusu fainali katika fainali zilizofanyika nchini Qatar mwaka 2022.

Baada ya mafanikio hayo Afrika imepata nafasi ya kupeleka wawakilishi 10 kwa mara ya kwanza baada ya FIFA kuongeza idadi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kutoka timu 32 hadi 48.

Huku ukiwa na Cape Verde watashiriki kwa mara ya kwanza kabisa, na DR Congo wakirejea kwenye mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.

Hata hivyo ndoto Afrika katika kusaka taji la kwanza inabebwa na makocha pamoja na wachezaji nyota kadhaa wa Kiafrika wanaotambaa katika klabu mbalimbali barani Ulaya, Asia na Afrika.

Miongoni mwa wachezaji wanaotazamwa zaidi na mashabiki kuibeba Afrika katika mashindano:

MASTA 01

1. Antoine Semenyo (Ghana)

Mshambuliaji huyu aliyezaliwa London amekosa ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na Manchester City, lakini alitoa pasi ya ushindi katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea mwezi uliopita kupitia ustadi mkubwa wa binafsi.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26 anaingia Kombe la Dunia akiwa ametoka kuwa na msimu bora zaidi wa kufunga mabao 17 katika Ligi Kuu England, saba kati ya hayo yakija baada ya kuhamia Manchester City mwezi Januari.

Kutokana na majeraha ya nyota wa Tottenham Hotspur, Mohammed Kudus, Semenyo anaweza kubeba matumaini makubwa ya Ghana.

Ghana itacheza dhidi ya England, Croatia na Panama katika Kundi L, huku Semenyo akitafuta bao lake la kwanza katika mashindano makubwa ya kimataifa.

MASTA 02

2. Yan Diomande (Ivory Coast)

Ivory Coast wanarejea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2014 wakiwa na wachezaji wengi vijana ambao ni bora zaidi duniani.

Diomande mwenye miaka 19 alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa Bundesliga baada ya kufunga mabao 12 na kutoa pasi nane za mabao, akiisaidia RB Leipzig kumaliza nafasi ya tatu na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kutokana na kiwango chake, amehusishwa na uhamisho wa thamani kubwa kwenda klabu kama Liverpool na Chelsea.

Uwezo wake mkubwa wa kupiga chenga na kushinda mapambano ya mtu mmoja mmoja unamfanya kuwa tishio kubwa kwa mabeki.

MASTA 03

3. Ronwen Williams (Afrika Kusini)

Afrka Kusini wanarejea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu walipoandaa mashindano hayo mwaka 2010.

Nahodha na kipa Ronwen Williams amekuwa maarufu kwa uwezo wake wa kuokoa mikwaju ya penalti, hasa baada ya kuokoa penalti nne katika ushindi dhidi ya Cape Verde kwenye robo fainali za AFCON 2023.

Mchezaji huyo mwenye miaka 34 pia amesaidia Mamelodi Sundowns kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, jambo lililoongeza uzoefu wake katika mechi kubwa.

Afrika Kusini itafungua mashindano dhidi ya wenyeji wenza Mexico kabla ya kucheza na Czech na Korea Kusini.

MASTA 04

4. Roberto Lopes (Cape Verde)

Beki wa kati Roberto “Pico” Lopes amekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya Cape Verde katika miaka ya hivi karibuni.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Ireland alialikwa kwa mara ya kwanza kuichezea Cape Verde kupitia ujumbe wa LinkedIn ambao mwanzoni aliupuuzia kwa sababu ulikuwa umeandikwa kwa Kireno.

Akiwa na miaka 33, Lopes alicheza karibu mechi zote za kufuzu Kombe la Dunia na kusaidia taifa hilo kufuzu kwa mara ya kwanza kabisa.

Cape Verde wako katika kundi gumu pamoja na Hispania, Uruguay na Saudi Arabia.

MASTA 05

5. Brahim Diaz (Morocco)

Nyota wa Real Madrid alikuwa mchezaji muhimu kwa Morocco katika AFCON 2025, akifunga mabao matano na kusaidia timu kufika fainali.

Hata hivyo, alikumbwa na wakati mgumu alipokosa penalti muhimu dhidi ya Senegal katika mchezo wa fainali.

Licha ya tukio hilo, Diaz atakuwa na hamasa kubwa ya kujithibitisha katika Kombe la Dunia.

Morocco wataanza kampeni yao dhidi ya Brazil kabla ya kukutana na Scotland na Haiti.

MASTA 06

6. Ismaila Sarr (Senegal)

Mchezaji huyu mwenye miaka 28 alikuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa na Crystal Palace, akifunga mabao 21, rekodi bora zaidi katika mafanikio yake.

Mabao tisa kati ya hayo yalikuja katika UEFA Conference Ligi, ambapo Palace walitwaa taji lao la kwanza la Ulaya.

Sarr atatarajia kuhamisha kiwango chake kizuri cha klabu hadi kwenye jukwaa la kimataifa.

Senegal itacheza dhidi ya Ufaransa, Norway na Iraq katika Kundi I.

MASTA 07

7. Omar Marmoush (Misri)

Licha ya kutokuwa na mwanzo mzuri kabisa baada ya kuhamia Manchester City kwa ada kubwa kutoka Eintracht Frankfurt, Marmoush bado ni mmoja wa nyota muhimu zaidi wa Misri.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 alifunga mabao mawili katika AFCON 2025 na sasa anatarajia kung’ara katika Kombe la Dunia lake la kwanza.

Misri, mabingwa wa Afrika mara saba, bado hawajawahi kushinda mechi yoyote ya Kombe la Dunia licha ya kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kushiriki mashindano hayo.

Kutokana na kurejea kwa nahodha Mohamed Salah kutoka majeraha baada ya msimu usioridhisha akiwa na Liverpool, kocha Hossam Hassan atahitaji Marmoush kuchukua jukumu la kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Mafarao.

Kwa ujumla, Kombe la Dunia 2026 linaweza kuwa jukwaa la Afrika kuandika historia mpya, huku nyota kama Semenyo, Diomande, Williams, Diaz, Sarr na Marmoush wakitarajiwa kuwa miongoni mwa sura kuu za bara hilo katika mashindano hayo.