Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Njia mpya za Simba CAF

NI sawa kusema tunaanzia pale tulipoishia msimu uliopita, baada ya asilimia kubwa ya kila kitu kuhusu Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kukamilika, kwani mambo yanaanza rasmi mapema mwezi ujao.

Msimu uliopita ulikuwa bora kwa Yanga ambayo ilianza vibaya kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kutolewa mwanzoni tu na kutupwa kwenye Kombe la Shirikisho na walifanikiwa kufika hatua ya fainali kwa mara ya kwanza kwao na Tanzania kwa jumla.

Kwa msimu huu mambo pia hayaonekani kuwa mabaya kwa kuwa timu hiyo pia imefuzu kwenda Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya pili.

Pamoja na Yanga timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu, Simba nayo imefuzu kwenda Ligi ya Mabingwa kama ilivyofanya kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo.

Msimu uliopita Tanzania ilifanikiwa kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa pamoja na kwamba nyingine zilishindwa kufanya vizuri lakini msimu huu kuna matumaini mambo yanaweza kuwa mazuri.

Pamoja na kufuzu kwao, lakini juzi picha halisi ya wapinzani wao ilionekana baada ya mataifa mengi kukamilisha timu zao zinazoshiriki michuano hiyo mikubwa.

Nchi 54, wanachama wa Caf zitaingiza timu zao kwenye michuano hii msimu huu na mataifa 12 ikiwemo Tanzania yataingiza timu mbili Ligi ya Mabingwa na Shrikisho mbili.

Ratiba nzima:

Ratiba ya michuano hiyo inaonyesha michezo ya kufuzu kwa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itapigwa Agosti 18-19 na marudio ni Agosti 25-26.

Hatua ya kwanza itapigwa Septemba 15-16 na marudio ni Septemba 25-26, baada ya hapo hatua ya makundi itaanza Desemba 1-2 na mwisho wa hatua hiyo ni Februari 27.

Robo fainali itakuwa Machi 15-16 na mechi ya pili Machi 29-30, nusu fainali Aprili 12-13 na 19-20 na fainali itapigwa Mei 12 mwaka 2024.

Wababe wa mbili mbili:

Pamoja na timu nyingi kuwa na ubabe wao kwenye michuano ya Afrika, lakini ukweli ni kwenye Ligi ya Mabingwa wababe wengi wamerejea na sasa wanataka tena heshima yao kwenye michuano hiyo.

Nchi za Kiarabu, Morocco, Algeria, Misri na Tunisia ni kati ya mataifa ambayo yamekuwa yakifanya vizuri kwenye michuano hii mikubwa Afrika.

Morocco, hili ni kati ya taifa linaloingiza timu mbili kwenye michuano hii na waliofuzu ni FAR Rabat ambao ndiyo vinara wa ligi hiyo, lakini Wydad nao wamefuzu kwa hatua hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi.

Tunisia hapa bingwa wake ni Étoile du Sahel ambaye ataungana na Esperance de Tunis kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa upande wa Misri wao mabingwa nin Al Ahly, ambao wataungana na Pyramids kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Kutoka Algeria, Simba na Yanga wajiandae kupambana na CR Belouizdad pamoja na CS Constantine, ambao wameshika nafasi ya kwanza na ya pili.

Afrika Kusini, kwao wapinzani ni wale waliozoeleka kwani zilizopata nafasi msimu huu ni Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns ambao msimu uliopita walikuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.

DR Congo, pamoja na kwamba ligi haikumalizika, lakini timu mbili zimepewa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa ambazo ni TP Mazembe pamoja na AS Vita na hivyo ni sehemu nyingine ambayo linaweza kutokea la kutokea kwa Simba na Yanga kwenda hapo.

Angola, hii ikiwa ni sehemu ngumu kwa wapinzani, kuna kigogo Petro de Luanda ambaye ameshafuzu kwa hatua hiyo, Primeiro de Agosto naye atashiriki michuano hiyo msimu huu baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili.

Vigogo wa Nigeria, Enyimba wamerejea tena kibabe baada ya kutwaa ubingwa wa nchi yao na msimu ujao watakuwa kwenye vita tena wakiwa pamoja na Remo Stars.

Nchi kadhaa vigogo ambazo zinaingiza timu moja moja ni mabingwa wake ni Power Dynamos Zambia, Coton Sport Cameroon,  Otôho d'Oyo Congo, Jwaneng Galaxy FC ya Botswana, Gor Mahia ya Kenya, Green Mamba FC ya Eswittin, Medeama Ghana, APR Rwanda na Vipers SC ya Uganda.