Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MWANUKE: Kuna Nyoni halafu Chama

Muktasari:

  • Si mwingine ni Jimmyson Mwanuke ambaye alijiunga na Simba akitokea Gwambina FC msimu wa 2021/22, licha ya timu mhiyo kushuka daraja msimu huo uwezo wake uliwashawishi viongozi wa Simba na kumnasa.

USAJILI wake ndani ya Simba ulizua maswali mengi licha ya uwezo alionao, lakini wengi walikuwa wanajiuliza atacheza nafasi gani hii ni kutokana na aina ya wachezaji waliokuwa ndani ya kikosi hicho.

Si mwingine ni Jimmyson Mwanuke ambaye alijiunga na Simba akitokea Gwambina FC msimu wa 2021/22, licha ya timu mhiyo kushuka daraja msimu huo uwezo wake uliwashawishi viongozi wa Simba na kumnasa.

Mwanaspoti limefanya naye mazungumzo kiungo huyo ambaye kwa sasa anacheza Fountain Gate amefunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna alivyoipokea ofa ya kutua Simba lakini pia amemtaja Erasto Nyoni kuwa ni mchezaji ambaye amekuwa sehemu ya mafanikio yake kutokana na kujifunza mengi kutoka kwake.


SIMBA ILIKUWA SAPRAIZI

Alikuwa na msimu mzuri ndani ya Gwambina ambayo licha ya kushuka daraja yeye aliyendelea kubaki ligi kuu kama anavyofunguka mwenyewe.

"Haikuwa matarajio yangu kutua Simba licha ya kuwa na msimu bora niliamini nitapata timu ya kucheza nje ya Gwambina lakini ghafla nilipata simu ya kutakiwa na Simba kwangu ilikuwa furaha kubwa sana," anasema na kuongeza;

"Nilipokea kwa furaha sana taarifa ya kutakiwa kucheza Simba na mara baada ya mipango kwenda kama ilivyopangwa na mimi kujiunga na Simba nilikuwa na furaha kubwa bila kujali changamoto nitakazokutana nazo nilichozingatia zaidi ni kuitumikia timu hiyo."

Mwanuke anasema hajawahi kujutia kufanya uamuzi wa kujiunga na Simba aliamini ni wakati wake sahihi kwani alikuwa kwenye kiwango bora licha ya kukosa nafasi ya kucheza kitendo cha kujiunga na timu hiyo mambo mengi yalibadilika.


PABLO ALIMBADILI NAMBA

Kila mchezaji anakuwa na matarajio makubwa kwenye timu anayoenda akiamini katika nafasi ambayo amemfanya awe bora alipotoka lakini mambo yanakuwa tofauti akifika timu nyingine kama anavyofunguka Mwanuke.

"Simba nilisajiliwa kama winga na kiungo mshambuliaji lakini kutokana na aina ya makocha waliopita na wao wana jicho lao la kuona nafasi mchezaji anaweza kufiti kutokana na mifumo yao nikajikuta nabadilishwa nafasi,"

"Ni ngumu kuweka wazi kuwa ni mchezaji gani alikuwa ananinyima nafasi ya kuchyeza ndani ya kikosi cha Simba kwani nakumbuka kocha Pablo Franco ndiye ambaye alinibadili nafasi nilicheza hadi beki chini yake lengo lake lilikuwa ni kuona napata nafasi na ni kocha ambaye alikuwa ananipa moyo sana kwamba nina kipaji kikubwa nipambane."

Anasema makocha wanatamani acheze lakini kwenye nafasi hiyo pia kuna mchezaji anataka kucheza hivyo alijikuta akitafutiwa nafasi kila eneo ili aweze kufiti kuingia kwenye mfumo lakini mambo hayakwenda vizuri hadi alipoamua kutoka kwa mkopo.

MAYELE, CHAMA, BOCCO

Tanzania imepita nyota wengi bora wa kigeni na wazawa ambao wameacha alama kwenye ligi kwa upande wa kiraka Mwanuke amewataja nyota watano bora kwake huku akiweka wazi kuwa kuna mambo makubwa wameyafanya na kuongeza thamani ya ligi.

"Ligi yetu kutajwa kwenye tano bora kwa ubora hawajakosea inastahili kuchanganywa kwa nyota wa ndani na kigeni kumekuza soka letu na kuboresha vipaji vya baadhi yetu ni wachezaji wengi wa ndani na nje wamefanya mambo makubwa," anasema na kuongeza;

"Ukisema nitaje baadhi sitaacha kumtaja Fiston Mayele, Chama, Chris Mugalu na Moses Phiri ni sehemu ya nyota bora wa kigeni waliofanya mambo makubwa kwenye ligi yetu na kuacha alama ni vipaji vikubwa ambavyo vinaendelea kuibwa kwenye ligi yetu."

Anasema kwa upande wa wachezaji wa ndani John Bocco amemtaja kuwa ndiye mchezaji mwenye rekodi nzuri kuanzia ligi kuu hadi timu ya taifa anastahili kuendelea kuenziwa licha ya kutokuwa na mwisho mzuri lakini amefanya vitu vingi bora ambavyo vimekuwa sababu ya vijana wengi kuamua kuingia kwenye soka.


KUCHEZA NA CHAMA, SOWAH

Wakati Shirikisho la Soka likiongeza nyota wa kigeni kutumika wote kwenye mechi moja huku na idadi ya kusajiliwa ikiongezeka kutoka nane hadi 12 Mwanuke amefunguka faida yake.

"Nimecheza Simba na Singida Black Stars kote nilikuwa na furaha lakini pia nafurahi kusema kuwa nilikuwa na wakati mzuri kufanya mazoezi na wachezaji wengi bora na wenye malengo makubwa hii ni sehemu ya mafanikio ukiondoa kucheza," anasema na kuongeza;

"Ukiondoa kuto kupata nafasi ya kucheza lakini nafasi ya kufanya mazoezi na nyota bora wenye uwezo mkubwa kimbinu na kiuchezaji kwangu ni mafanikio makubwa kwani kuna vitu nilikuwa navipata na sasa navifanyia kazi."

Mwanuke anasema licha ya mengi kuzungumzwa kwa wachezaji wanaokaa benchi kwa timu kama Simba na Singida Black Stars kuna manufaa wanayapata na wanapopata nafasi ya kutoka na kujiunga na timu nyingine wanafanyia kazi yale waliyojifunza.

Kiraka huyo akiwa Simba amecheza na nyota wengi wa kigeni kwenye uwanja wa mazoezi akiwemo Chama hivyo hivyo kwa upande wa Singida Black Stars amefanya mazoezi pamoja na Jonathan Sowah akiwa Singida kabla ya msimu huu kujiunga na Simba.

KIRAKA ILA WINGA HATARI

Sio wachezaji wote wanaweza kucheza nafasi nyingi uwanjani kuna ambao wanacheza nafasi moja na kuna ambao wanajikuta wakibadilishwa nafasi na kujikuta wanamudu kucheza nafasi mbili kama ambavyo anafunguka Mwanuke.

''Naweza kucheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani lakini nafurahi zaidi nikichezeshwa eneo la winga ambalo ndilo nililokuwa nikilicheza kwenye timu nyingi numa lakini sasa naweza kucheza nafasi zaidi ya mbili kutokana na na makocha wanavyoamua kunitumia,"

"Nabadilika kutokana na mfumo wa kocha na namna anavyotaka nicheze wachezaji wengine hawawezi kubadili nafasi lakini mimi nimeweza na nafurahia kuwa mchezaji ambaye naweza kucheza maeneo mengi inanipa nafasi ya kupata namba ya kucheza.''

Anasema akicheza eneo la winga anakuwa huru zaidi kufanya maamuzi na anatumia kasi aliyonayo kufika haraka eneo la wapinzani ndio maana amekuwa akifurahia zaidi akipangwa nafasi hiyo. lakini anakutana na changanmoto ya kubadilishwa namba kutokana na makocha anaokutana nao.


NYONI, CHAMA WANANIONGOZA

Kwa nyota wanaocheza ligi ya ndani na mzawa huwezi kusita kutaja jina la Erasto Nyoni ambaye ni kiraka na amekuwa akifanya vizuri kila eneo analopangwa kama anavyofunguka Mwanuke.

''Kuna wachezaji wengi ambao wananivutia lakini nimekuwa nikimtazama zaidi Erasto Nyoni ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na anauezo wa kucheza nafasi nyingi na kwa ubora,"

''Kwa nyota wa kigeni kuna mchezaji fundi anaitwa Clatous Chama huyu mpira unamtii anaufanya anachokitaka kwa ubora ni miongoni mwa wachezaji ambao nimepata bahati ya kucheza nao na nimenufaika na mengi kwa kujifunza kutoka kwake."

Mwanuke anasema kutokana na kuwa na machaguo mengi ya kucheza ukionyoa wachezaji hao pia amekuwa akivutiwa na wachezaji wengi ambao akisema amtaje mmoja mmoja hataweza kumaliza lakini kwa upande wake ni mchezaji ambaye anaamini katika kujifunza zaidi.

PACOME KUNA MUKONO

Wakati wadau na baadhi ya wachezaji wanao cheza ligi kuu bara wakimtaja Pacome Zouzoua kwa ubora kutokana na namba na aina ya uchezaji wake kwa upande wa Mwanuke amemtaja Eli Mukono kuwa ni fundi sana wadau wamtupie jicho.

"Sikatai kuna wachezaji wengi bora kwenye ligi yetu na wanafanya vizuri lakini kwangu Mukono ni kiungo bora sana anafanya vizuri ndani ya Fountain Gate na ligi kwa ujumla," anasema Mwanuke ambaye anavaa jezi namba 14 aliyoitaja kuwa ni tarehe ya kuzaliwa kwake.

"Ukiondoa huyo kwa upande wa nyota wa ndani ambao wanafanya vizuri eneo la kiungo ni Ismail Aziz Kadar pia ni kiungo mzuri sana anafanya vizuri nimekuwa nikimzingatia sana na kuchukua mazuri kutoka kwake." anasema kuwa mara nyingi amekuwa akivutiwa na wachezaji anaocheza nao timu moja kwa sababu wanampa ushindani lakini pia ata nje ya timu yake anajifunza kutoka kwa wengine.