Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwana FA, Msigwa nyie bado familia

FAMILIA Pict

Muktasari:

  • Jana ghafla Rais Samia Suluhu Hassan akafanya mabadiliko ya wizara mbalimbali na mojawapo iliyoguswa ni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

MAISHA ya kuteuliwa na kutenguliwa ni ya kawaida katika taasisi za serikali na ni jambo ambalo linatokea mara kwa mara.

Jana ghafla Rais Samia Suluhu Hassan akafanya mabadiliko ya wizara mbalimbali na mojawapo iliyoguswa ni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aliyekuwa Naibu Waziri, Mwana FA akabadilishwa kwa kuhamishiwa katika Wizara ya Uvuvi ambako anaenda kuwa waziri kamili.

Na aliyekuwa Katibu Mkuu, Gerson Msigwa naye akapata uhamisho kwenda katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum.

Tunajua majukumu yatawabana huko katika wizara ambako wamepelekwa lakini kwa vile wao ni watu wa michezo, tunawaomba waendelee kuwa sehemu ya familia ya michezo na wasiitupe moja kwa moja.

Tumeona kazi kubwa waliyoifanya katika kusaidia maendeleo ya michezo kila mmoja kwa wakati wake hasa katika kuipaisha Tanzania kimataifa.

Sisi hapa kijiweni tunaamini na tunatamani kuona Mwana FA na Msigwa wakiendelea kuwa familia kwa uahauri na maoni na pia kujitokeza katika matukio mbalimbali ya kimichezo.

AFCON 2027 inakuja na wao wawili kwa kiasi kikubwa walishiriki katika mapambano ya kuhakikisha Tanzania inafanya maandalizi ya uhakika kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yataanza Juni mwakani.

Huko katika wizara walikoenda tunawategemea wawe mabalozi wazuri wa kushawishi walio chini yao kuipa sapoti kubwa AFCON 2027.