Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tamasha la Utamaduni Morogoro lawaibua wadau

UTAMADUNI Pict
UTAMADUNI Pict

Viongozi wa mila na wadau mbalimbali wamesema pamoja na kuwa na tamasha la kitaifa la utamaduni, lakini ipo haja kwa Serikali kuweka utaratibu kwa kila mwaka kuwa na tamasha hilo kwenye mikoa yote hapa nchini ili wananchi waweze kukumbushwa tamaduni zao.

Akizungumza kwenye tamasha la nne la utamaduni ambalo kitaifa linafanyika mkoani Morogoro, kiongozi wa mila kutoka Mkoa wa Pwani, Hadija Nyambasi amesema ni vyema kila mkoa ungekuwa na siku maalumu ya kuadhimisha siku ya utamaduni ili kutoa fursa kwa makabila kushiriki na kuonesha tamaduni na mila zao.

"Pamoja na kuandaa tamasha la kitaifa, lakini ni vyema Serikali iweke utaratibu wa kila mkoa kuandaa tamasha lake, hii itatoa fursa kwa makabila yote kuonesha mila, tamaduni na desturi zao, nchi hii ina makabila zaidi ya 160, kutokana na uwezo wa kifedha sio rahisi yote kushiriki kwenye tamasha moja la kitaifa, lakini wanaweza kushiriki kwenye mikoa yao," amesema Nyambasi.

UTAM 01

Ameongeza kuwa: "Mfano Mkoa wa Pwani una makabila zaidi ya kumi, sio rahisi yote kufika kwenye tamasha hili la kitaifa lakini kama Serikali ya mkoa ingeandaa tamasha lao, makabila hayo yote yangeweza kushiriki na watu wa Pwani wangeona utamaduni wao."

Naye kiongozi wa mila kutoka Kabila la Wagogo, Michael Chisima, amesema tamasha hilo lingeandaliwa kama zinavyoandaliwa sherehe nyingine za kitaifa ambazo pamoja na kufanyika kitaifa lakini pia zimekuwa zikifanyika kwenye Kila mkoa ama kanda.

"Mfano maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi, siku ya wanawake au maonesho ya wakulima nane nane, kumekuwa na utaratibu wa sherehe hizo kufanyika kitaifa kwenye mkoa husika lakini pia sherehe hizo zimekuwa zikifanyika kwenye kila mkoa au kila kanda, hivyo utaratibu huo unaweza pia kufanyika kwenye maonesho ya tamasha la utamaduni," amesema Chisima.

"Sisi tupo hapa kwenye tamasha la kitaifa la utamaduni tunaonesha mila na utamaduni wa watu wa Dodoma, lakini kuna watu tumewaacha kule Dodoma wenye kabila lao hawapati fursa ya kuona mila zao, lakini kama kungewa na tamasha lingine la utamaduni la mkoa ambalo linaoneshwa huko Dodoma watu wa makabila ya Dodoma wangeshiriki na wangeona mila zao," amesema Chisima.

UTAM 02
UTAM 02

Ameongeza: "Nashauri hili tamasha la kitaifa liwepo kila mwaka ambapo kutakuwa na mzunguko mfano mwaka huu kimefanyika hapa Morogoro basi mwakani linaweza kufanyika mkoa mwingine lakini pamoja na kuwepo kwa tamasha hili la kitaifa kuwe na utaratibu wa kula mkoa kuandaa tamasha lake ambalo litafanyika kwa ngazi ya mkoa."

Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliofika katika tamasha hilo kutoka mkoani Kilimanjaro, Aziz Msuya ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuandaa tamasha hilo ambalo limekutanisha makabila mbalimbali na tamaduni zao.

"Mwaka huu tamasha linafanyika mkoani Morogoro, watu wa Morogoro wanaona mila na tamaduni zao kupitia tamasha hili, lakini baada ya tamasha hili hakutakuwa na jukwaa lingine kwa watu hawa wa Morogoro la kuwakumbusha haya wanayoyaona mpaka ipite miaka mingi ndiyo tamasha hili lije tena Morogoro," amesema Msuya.

Awali kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, aliwashauri wazazi na walezi kujenga utaratibu wa kuwapeleka watoto wao kwenye vijiji vyao kuona asili ya makabila yao, vitu vya kihistoria, vyakula vya asili, ngoma lakini pia waweze kujifunza lugha zao za asili.

Tamasha hilo la nne la kitaifa la utamaduni ambalo limekutanisha makabila yote ya Tanzania yanayoonesha mila na utamaduni wao ikiwemo mavazi, vyakula, ngoma na michezo ya asili, limezinduliwa Agosti 26, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima na litafungwa Agosti 29, 2026.