Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka mitano na maajabu kwa Mayele

MAYELE Pict


WANANGU mnapambana sana, pengine kwa muda huu upo zako kariakoo umeshika simu yako baada ya shughuli nzito ya kubeba mizigo, inawezekana muda huu umetulia kivulini baada ya kukimbizana na upepo kwa bodaboda yako tangu asubuhi.


Inawezekana tumbo lako linaunguruma kwa njaa lakini unachanganya udongo umpe fundi muendelee kujenga kwa sababu ndio kazi inayokupa kipato.


Wengine inawezekana mmechoka sana, lakini wosia wangu ni mmoja tu tusikate tamaa.

Katika Mitaa ya Ruo Oshwe, Kinshasa, Fiston Mayele akiwa na umri wa miaka 26, alionekana akitembea lakini hakuna mtu aliyesimama kumshangaa. Hakuna aliyemzingatia. Labda kwa sababu hawakuiona kesho yake. Hawakujua nini kitakuja kutokea kuanzia kipindi hiko hadi sasa.

MAYE 01

Ndo hivyo. Hakuna aijuae kesho. Hata Mayele mwenyewe hakuijua kesho yake. Hata hivyo, kwa sasa imeonekana.

Katika safu ya ushambuliaji ya timu ya taifa ya Congo, pale mbele hulikosi jina lake. Alianza kutamba na Ligi Kuu Bara akiingia bila ya kupewa nafasi kubwa ya kuwa shujaa, lakini aliondoka akiacha gumzo kuhusu kiwango chake.

Akaenda zake Pyramid ya Misri. Kuna aliyedhani ataibuka shujaa huko? Hapana. Akaibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hii ni maana halisi ya maajabu katika maisha. Mambo yote hayo aliyoyafanya ni ndani ya miaka mitano tu. Wapo wachezaji wengi hutumia zaidi ya miaka 10 kujiwekea ufalme, lakini kwa Mayele, ni kama alichelewa kutokana na kuzidi kuwa bora licha ya umri kumtupa mkono.

MAYE 02

Akiwa na miaka 31 sasa, bado hajakata tamaa na miguu yake imeendelea kudhihirisha ubora wake.

Kuna stori zinaeleza hata wakati anasajiliwa na Yanga, hakukuwa na imani kubwa juu yake, alionekana mchezaji wa kawaida tu, hakuna CV kubwa, hakuwa anagombaniwa, ni kama mtu aliyesuswa tu.

Wakala wake alituma video kwa watu mbalimbali Dar es salaam, wengi walizitazama na kuweka kapuni, ni Nassredine Nabi ndio aliamua kukata mzizi wa fitina akaamua kumwamini na baada ya hapo kila kitu kimebadilika.

Leo Mayele akirudi DR Congo, hawezi tena kutembea kama alivyokuwa anatembea awali. Akifanya hivyo kila wakati itambidi asimame apige picha na watu, sikwambii hapa Tanzania.

Leo akiamua apige simu AS Vita anataka kurudi, atapokelewa kwa mapokezi ya kifalme na ndio atakuwa mchezaji staa wa timu, lakini miaka mitano nyuma hakuwa hata akipewa kipaumbele katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

MAYE 03

Kule katika ardhi ya Farao na mtumishi wake Haaman, mabosi wamiliki wa visima vya mafuta huwaambii kitu kuhusu Mayele, inawezekana miaka mitano nyuma kama ingetokea wakala mmoja amependekeza jina lake, pengine wasingejisumbua hata kufungua ujumbe wake wa Whatsapp. Leo Ukitaka kumnunua Mayele Pyramid utahitaji zaidi ya Dola 1 milioni.

Maisha yanaenda kasi sana. Inawezekana umekata tamaa kabisa, unafikiria huwezi kufanikiwa tena kutokana na umri wako, lakini maajabu yamewekwa na Mungu ili yatokee na ikiwa unabisha tazama yale yaliyomtokea Mayele.

Wakati anakuja Tanzania hakukuwa na aliyetarajiwa muda na wakati huu angekuwa amefanikisha hayo aliyofanikisha. Lakini sasa ametimiza na hata wakati anaondoka kila mtu alikuwa akililiwa.

Muulize shabiki wa timu yoyote kati ya zile za mitaa ya Kariakoo na Jangwani kuhusu staa huyu, hakuna atakayethubutu kukwambia hatamani kumwona kwenye timu yake.

MAYE 04

Wakati umri wake ukizidi kukata mbuga, sasa akiwa na miaka 31, Mayele ameendelea kuzivunja rekodi, ameendelea kuwindwa ameendelea kutamaniwa.

Inawezekana kuwa muda alilia kwa kuona wenzake wakiondoka na kumwagika, Ubelgiji, timu kubwa Afrika na Ulaya kwa jumla, lakini sasa ni muda wake wa kufurahi.

Miezi kadhaa iliyopita, kulikuwa na ofa nyingine kutoka timu za Uarabuni. Zilihitaji saini yake na ziliweka mpunga wa kutosha. Pyramid ilimzuia kwa sababu wanaamini hiyo ndio injini yao. Ajabu hii kwa mchezaji aliyekuwa kama akiba AS Vita akiwa na miaka 26.


REKODI ZA MIAKA MITANO

Katika mashindano ya FIFA Intercontinental Cup inayoendelea sasa katika hatua ya mtoano, Mayele ndiyo anaongoza katika orodha ya ufungaji bora baada ya kutupia mabao matatu katika mchezo dhidi ya Al Ahli ya Saudi Arabia iliyokuwa na mastaa kibao ikiwemo Ivan Toney kutoka England.

Katika michuano hiyo, Pyramid ipo katika hatua ya mwisho na ikishinda itakutana na Paris Saint-Germain katika mchezo wa fainali.

Amefika fainali mbili za mashindano makubwa ya CAF kwa ngazi ya klabu, akianza na Yanga msimu wa 2022/23 katika Kombe la shirikisho Afrika ingawa walipoteza mbele ya USM Alger.

Mayele pia alifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita akiwa na Pyramid na kufanikiwa kushinda taji hilo kwa kuichapa Mamelodi Sundown kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

Katika msimu huo pia Mayele alifanikiwa kushinda tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo akiweka kambani mabao sita.

Mbali ya mataji mawili ya Ligi Kuu bara, mawili ya kombe la FA akiwa na Yanga, tangu ajiunge na Pyramid Mayele amechukua matatu ya michuano mbalimbali, moja likiwa la ndani.

Katika timu ya taifa, kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka alifanikiwa kucheza michuano ya AFCON akiwa na DR Congo mwaka jana.